Iran: Watoto laki tatu wa Afghanistan wanasomeshwa bure hapa nchini
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i43198-iran_watoto_laki_tatu_wa_afghanistan_wanasomeshwa_bure_hapa_nchini
Naibu Waziri wa Elimu nchini Iran amesema kuwa, jumla ya watoto laki mbili na 93 elfu 366 raia wa Afghanistan wanasoma elimu ya msingi katika shule mbalimbali nchini hapa.
(last modified 2026-03-27T07:58:19+00:00 )
Apr 16, 2018 22:48 UTC
  • Iran: Watoto laki tatu wa Afghanistan wanasomeshwa bure hapa nchini

Naibu Waziri wa Elimu nchini Iran amesema kuwa, jumla ya watoto laki mbili na 93 elfu 366 raia wa Afghanistan wanasoma elimu ya msingi katika shule mbalimbali nchini hapa.

Rezvan Hakim Zadeh ameyasema hayo Jumatatu alipokutana na Hossein Ali Hosseini, Katibu wa Kwanza wa Ubalozi na Mkuu wa Kitengo cha Elimu na mafunzo wa Afghanistan nchini Iran na kuongeza kuwa, kubadilishana tamaduni na mafunzo kati ya Iran na Afghanistan ni suala ambalo litapelekea kupanuliwa zaidi mahusiano ya pande mbili. 

Naibu Waziri wa Elimu wa Iran amesema kwamba katika mwaka wa masomo wa 2017-2018 jumla ya wanafunzi laki tatu 22 elfu na 450 raia wa Afghanistan walikuwa wanaenda shule mbalimbali hapa nchini na kongeza kuwa, kiwango hicho cha wanafunzi kinajumuisha asilimia 91 ya watoto wa raia wa kigeni wanaoenda shule na waliofikia umri wa kwenda shule nchini hapa.

Rezvan Hakim Zadeh, Naibu Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya Msingi kilicho chini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo nchini Iran

Kadhalika Rezvan Hakim Zadeh ameashiria amri ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran Ayatullahil-Udhma Sayyid Ali Khamenei kuhusu ya udharura wa kuwasajili watoto wa rai wa kigeni katika shule za Iran na kusema kuwa amri ya Kiongozi Muadhamu inalenga usawa wa wanadamu wote wa kupata haki ya kusoma na kupata elimu hususan watoto na kwamba katika uwanja huo hakuna tofauti kati ya watoto wa Iran au raia wa kigeni.

Amesisitiza kwamba, ushirikiano wa kielimu kati ya nchi mbili za Afghanistan na Iran utaimarisha ushirikiano wa kistratijia na endele baina ya pande mbili.

Raia wa Afghanistan wanaume na wanawake wakipatiwa masomo katika Chuo Kikuu cha al-Muustafa mjini Qom

Maafisa kadhaa wa Umoja wa Mataifa wamekuwa wakiipongeza na kuishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kutokana na moyo wake wa upendo wa kuwapatia elimu wakimbizi waliopo nchini na kusisitiza kuwa, serikali ya Iran imewafungulia wakimbizi wa nchi tofauti milango ya shule za msingi, sekondari, vyuo vikuu, hospitali na hata mipaka yake, kiasi kwamba wakimbizi hao wamekuwa wakipewa haki sawa na raia wa Iran.

Watoto wa Afghanistan wakiwa katika shule za msingi nchini Iran

Mwaka jana Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) mbali na kuishukuru Iran lilisema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ni nchi ya nne duniani yenye idadi kubwa zaidi ya wakimbizi na kuongeza kuwa, ukarimu wa nchi hii kwa wakimbizi ni mfano wa kuigwa na mataifa mengine duniani.