May 16, 2018 14:06 UTC
  • Rais wa Iran: Michezo ya kisiasa haiwezi kuitenganisha Quds na Waislamu

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Mji wa Quds au Baitul Muqaddas (Jerusalem) ambako ndiko uliko Msikiti wa Al Aqsa ni mji unaoheshimiwa na Waislamu wote na hivyo ardhi hiyo takatibu haiwezi kuteganishwa na Waislami zaidi ya bilioni moja na nusu duniani kwa mchezo wa kisiasa.

Rais Rouhani ameyasema hayo leo katika kikao cha Baraza la Mawaziri huku akiashiria mapambano na muqawama wa watu wa Palestina na kuongeza kuwa: "Utawala wa Kizayuni unaendeleza uvamizi na mauaji ya watu wasio na hatia." Rais Rouhani ameongeza kuwa katika Siku ya Nakba wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamewahujumu wananchi madhulumu wa Palestina na kuua shahidi idadi kubwa huku maelfu ya wengine wakijeruhiwa.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amebainisha masikitikio yake kuhusu kimya cha baadhi ya nchi za Kiarabu na Kiislamu kufuatia jinai za Wazayuni na kuongeza kuwa ni jambo la kusikitisah kuwa wakati taifa la Palestina linapambana kukomboa ardhi zake, baadhi ya nchi za Kiarabu zinatamka kuwa eti jinai za utawala wa Kizayuni ni hatua ya halali ya kuhijami.

Maandamano ya Wapalestina katika Siku ya Nakba

Rais wa Iran ameashiria kuendelea mapambano ya Wapalestina na kusema Waislamu duniani hawana njia nyingine ila kuungana katika kupambana na utawala wa Kizayuni wa Israel na kuwasaidia Wapalestina wapate ushindi.

Kwingineko katika matamshi yake, Rais Rouhani ameashiria Marekani kujiondoa katika mapatano ya nyuklia ya Iran yanayojulikana kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekeelzwahi na kusema: "Katika kadhia ya nyuklia baadhi wanadhani kuwa, mashinikizo, vikwazo, vitisho na hata kutoa ishara za vita ni mambo yanayoweza kulifanya taifa la Iran lisalimu amri lakini kusimama kidete na mapambano ya taifa la Iran ni dalili nzuri kuwa fikra hizo si sahihi na ni ghalati."

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema fikra za umma katika ulimwengu wa Kiislamu hakuna waungaji mkono wa Marekani isipokuwa katika tawala chache ndogo zinzopinga mageuzi katika eneo na utawala ghaisbu wa Kizayuni.    

Tags