Tehran: Marekani inapaswa kuliomba radhi rasmi taifa la Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i47341-tehran_marekani_inapaswa_kuliomba_radhi_rasmi_taifa_la_iran
Waziri wa Mambo wa Ndani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Marekani inapaswa kuheshimu ahadi zake katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA na iliombe radhi rasmi taifa la Iran.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Aug 09, 2018 23:23 UTC
  • Tehran: Marekani inapaswa kuliomba radhi rasmi taifa la Iran

Waziri wa Mambo wa Ndani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Marekani inapaswa kuheshimu ahadi zake katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA na iliombe radhi rasmi taifa la Iran.

Abdolreza Rahmani Fazli amesema hayo mkoani Yazdi, (katikati mwa Iran) na huku akigusia uadui wa waziwazi wa Marekani dhidi ya taifa la Iran na kujitoa kwake kinyume cha sheria katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA ameongeza kuwa, viongozi wa Marekani hawana mwamana hata kidogo na kufanya mazungumzo mapya na Marekani ni jambo lisilowezekana.

Rais wa Marekani, Donald Trump

 

Vile vile amesema, kitendo cha Marekani cha kujitoa katika mapatano ya kimataifa ya JCPOA na kukataa majirani wa Iran na nchi nyingi duniani kufuata siasa hizo za Marekani kumeandaa mazingira ya wazi zaidi ya ushirikiano ujao wa kiuchumi baina ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na nchi nyingine duniani.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran aidha amesema, daima viongozi wa Marekani wanafanya njama za kuidhoofisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kuongeza kuwa, baada ya kupita miaka 40 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu haiwezekani tena kuitisha Iran kwa vikwazo vya mafuta.

Vile vile amesema, adui anatumia nguvu zake za kipropaganda kujaribu kuzusha fitna na machafuko ndani ya Iran na ndio maana linapotokezea tatizo dogo tu humu nchini, utaona mabanda ya propaganda ya adui yanalikuza kupindukia suala hilo.