Vijana wanamapinduzi wa Iran wataka kuimarishwa Umoja wa Kiislamu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i49043-vijana_wanamapinduzi_wa_iran_wataka_kuimarishwa_umoja_wa_kiislamu
Vijana wanamapinduzi wa Iran wametoa wito wa kuimarishwa Umoja na mshikamano katika ulimwengu wa Kiislamu na kukabiliana na njama za Marekani na Israel.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Oct 26, 2018 01:19 UTC
  • Vijana wanamapinduzi wa Iran wataka kuimarishwa Umoja wa Kiislamu

Vijana wanamapinduzi wa Iran wametoa wito wa kuimarishwa Umoja na mshikamano katika ulimwengu wa Kiislamu na kukabiliana na njama za Marekani na Israel.

Risala iliyosambazwa na vijawa wanamapinduzi wa Iran kwa lugha kadhaa imesema, kuna udharura wa kutolea mapendekezo na mitazamo mbalimbali juu ya hatua za kimatendo za kuimarishwa umoja na mshikamano baina ya wasomi na wanafunzi wa vyuo vikuu wa Kiislamu.

Risala hiyo imesisitiza kuwa, ushirikiano na kubadilishana mawazo baina ya vijana Waislamu unaweza kuwa dirisha jipya la maendeleo, nguvu na uwezo wa Umma wa Kiislamu katika masuala ya sayansi na ya kiroho. Risala hiyo imesema miongoni mwa changamoto kubwa za kipindi cha sasa ni usalama wa ulimwengu wa Kiislamu na kwamba, Marekani na utawala haramu wa Israel zinatumia ugaidi katika fremu ya makundi ya kitakfiri ya Daesh na al Qaida kwa ajili ya kuchafua sura halisi ya Uislamu.

Risala hiyo imesisitiza kuwa, kuna udharura wa kuchukuliwa hatua za kivitendo za kuzuia madhara ya njama hizo kwa mataifa ya Waislamu kwa kuimarisha umoja na mshikamano.