'Hakuna dola lolote linaloweza kuidhuru Iran'
(last modified Wed, 06 Mar 2019 02:53:42 GMT )
Mar 06, 2019 02:53 UTC
  • 'Hakuna dola lolote linaloweza kuidhuru Iran'

Msaidizi wa Amiri Jeshi Mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: "Hakuna dola lolote nje ya eneo linaloweza kuidhuru Iran."

Meja Jenerali Yahya Rahim Safavi ambaye pia ni  Mshauri wa Ngazi za Juu wa Amiri Jeshi Mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliyasema hayo Jumanne mjini Tehran alipowahutubia wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Maafisa wa Kijeshi cha Imam Hussein AS ambapo amebainisha kuwa, Iran haijawahi kuwa tishio kwa nchi yoyote ya Waislamu. Ameendelea kusema kuwa: "Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hivi sasa imebadilika na kuwa dola lenye nguvu zaidi katika eneo la Asia Magharibi na nchi hii ina taathira katika mlingano wa kimataifa"

Meja Jenerali Yahya Rahim Safavi, ambaye aliwahi kuwa Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ameashiria kudidimia na kudhoofika nguvu za Marekani na kusema: "Wamarekani wanafahamu kuwa wamedhoofika na wao si dola tena lenye nguvu zaidi duniani." Ametoa mfano na kusema, kama watawala wa Marekani wangekuwa na uwezo, wangelikwisha iangusha serikali ya Rais Bashar al Assad wa Syria.

Rais Bashar al Assad wa Syria (kushoto) akiamkuana na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Khamenei mjini Tehran mnamo February 25, 2019

Meja Jenerali Safavi amegusia pia nguvu mpya za Ulimwengu wa Kiislamu kitovu chake kikiwa ni Mapinduzi ya Kiislamu na kusema: "Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yalivuruga mlingano wa nguvu dunaini na sasa  kitovu cha mwamko wa kifikra katika Ulimwengu wa Kiislamu ni Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na uongozi wa Jamhuri ya Kiislamu."

Tags