Vikwazo dhidi ya Zarif; upinzani wa kimataifa dhidi ya Marekani
Hatua ya Marekani kumuwekea vikwazo Muhammad Jawad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekabiliwa na upinzani mkali wa jamii ya kimataifa, hatua ya kisiasa ambayo imekosolewa hata ndani ya Marekani kwenyewe.
Wizara ya Fedha ya Marekani imeweka jina la Muhammad Jawad Zarif katika orodha ya nchi hiyo ya mashirika na watu waliowekewa vikwazo, hatua ambayo imelaaniwa na kukosolewa na jamii ya kimataifa na hivyo kuonyesha kwa mara nyingine tena jinsi Marekani imetengwa katika ngazi za kimataifa.
Baada ya Marekani kutangaza hatua hiyo ya kisiasa ya kumuwekea vikwazo Muhammad Zarifi, Umoja wa Ulaya, China na Russia ambazo ni pande muhimu za mapatano ya kimataifa ya nyuklia yanayojulikana kama JCPOA zimesisitza kwamba zitaendelea kushauriana na kushirikiana na Waziri huyo Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Upinzani wa kimataifa dhidi ya hatua za upande mmoja za Marekani na zinazokwenda kinyume na taratibu zilizozoeleka kimataifa, ambazo zimekuwa zikichukuliwa na serikali ya Washington tokea Rais Donald Trump aingia madarakani nchini humo, umebadilika na kuwa msingi muhimu katika ngazi za kimataifa na bila shaka udiplomasia athirifu na hai wa Iran umekuwa na nafasi muhimu katika uwanja huo.
Udiploamsia wa wazi, wa kimantiki na unaofungamana na misingi ya maadili ya Kiislamu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran umepokelewa na kukubalika na Walimwengu na bila shaka upinzani unaoonyeshwa katika pembe tofauti za dunia dhidi ya siasa za mabavu na za upande mmoja za serikali ya Trump dhidi ya Iran ni thibitisho la wazi la ukweli huo.
Kufungamana na sheria za kimataifa na kuzingatia misingi pamoja na mifumo iliyojengeka juu ya fikra za pande kadhaa duniani, kumeifanya Jamhuri ya Kiisamu kuwa nchi inayowajibika kuhusiana na majukumu yake ya kimataifa, mfano wa wazi ukiwa ni kuheshimu kwake mapatano ya kimataifa ya JCPOA licha ya uvunjaji ahadi unaofanywa na nchi za Magharibi, zikiongozwa na Marekani ambayo imetupitia mbali na kujitoa kwa upande mmoja katika mapatano hayo muhimu ya kimataifa.
Diplomasia athirifu ya Iran katika ngazi tofauti za kimataifa imeifanya serikali ya Trump ikabiliwe na changamoto muhimu na bila shaka kuwekewa vikwazo Muhammad Zarif na serikali hiyo kunaonyesha wazi jinsi diplomasia hiyo imekuwa na taathira chanya katika upeo wa kimataifa. Uwezo mkubwa wa kubainisha mambo, kudhibiti kikamilifu elimu na mbinu za siasa pamoja na uwezo mkubwa wa kuukinaisha upande wa pili alionao Waziri Zarif, umezifanya siasa za mantiki za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zikubalike kirahisi ulimwenguni. Chombo cha diplomasia cha Iran kikiongozwa na Waziri Muhammad Jawad Zarif kupitia mashauriano muhimu, mazungumzo atharifu na vyombo muhimu vya habari na hasa vya Marekani pamoja na kutekeleza sheria za kimataifa, kimevuruga kabisa siasa haribifu za serikali ya Trump dhidi ya Iran na kuzifanya zisiwe na athari yoyote ya maana.
Katika mazingira hayo ni wazi kuwa kwa kuamua kumuwekea waziri huyo vizingiti vya kidiplomasia na sasa vikwazo, serikali ya Trump imekata kabisa tamaa kuhusiana na suala zima la Iran
Gazeti la Marekani la Washington Post liliandika jana Ijumaa kuhusiana na hatua ya serikali ya Trump kumuwekea vikwazo Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran kwamba: Haijulikana vyema ni uhusiano gani uliopo kati ya kumuwekea vikwazo Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran na malengo ya Marekani. Sababu inayokaribia ukweli ni kwamba hatua hiyo imechukuliwa kutokana na hasira ya serikali ya Marekani kuhusiana na mahojiano ya mara kwa mara anayoyafanya Zarif na vyombo vya habari vya Marekani mjini New York.
Majid Takht Rawanchi, Mwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa pia amesema: Vikwazo dhidi ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran haviwezi kuzima maneno ya Zarif yaliyo bayana na yenye hoja madhubuti.
Uungaji mkono wa jamii ya kimataifa kwa mapatano ya JCPOA na upinzani dhidi ya vikwazo na siasa za upande mmoja za Marekani dhidi ya taifa la Iran, yote hayo ni mambo yanayothibitisha wazi mafanikio ya diplomasia ya Jamhuri ya Kiislamu na bila shaka sauti ya diplomasia hiyo haiwezi kuzimwa kwa vikwazo wala kuwekwa vizuizi vya kidolomaisa katika njia ya Muhammad Jawad Zarif.
Kabla ya hapo pia Marekani ilishindwa kubuni mrengo wa upinzani dhidi ya Iran katia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa shabaha ya kuvunja mapatano ya JCPOA, jambo linalothibitisha wazi usahihi wa diplomasia ya Iran, diplomasia ambayo mafanikio yake yamekwamisha na kuichanganya kabisa Marekani katika njama zake za kueneza chuki na uhasama dhidi ya Iran.