Lavrov akaribisha ubunifu wa Iran kuhusu eneo la Ghuba ya Uajemi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i56385-lavrov_akaribisha_ubunifu_wa_iran_kuhusu_eneo_la_ghuba_ya_uajemi
Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia ametoa wito wa kupewa mazingatio zaidi pendekezo lililotolewa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusiana na eneo la Ghuba ya Uajemi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 03, 2019 00:45 UTC
  • Lavrov akaribisha ubunifu wa Iran kuhusu eneo la Ghuba ya Uajemi

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia ametoa wito wa kupewa mazingatio zaidi pendekezo lililotolewa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusiana na eneo la Ghuba ya Uajemi.

Sergey Lavrov amesema, eneo la magharibi mwa Asia limekuwa sawa na medani yenye hatari kubwa na kusisitiza kuwa, pendekezo lililotolewa na Iran kuhusu lango bahari la Hormuz linapaswa kupewa mazingatio. 

Kuhusu kadhia ya Syria, Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema kuwa: Wasyria wanapaswa kufikia makubaliano juu ya katiba mpya ya nchi yao bila ya uingiliaji kati wa nchi za kigeni. 

Ni vyema kukumbusha hapa kuwa, katika hotuba yake kwenye mkutano wa 74 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York siku chache zilizpita, Rais Hassan Rouhani wa Iran aliweka wazi misimamo ya Tehran kuhusu masuala ya kikanda na kimataifa na kutoa pendekezo la kuimarisha amani lililopewa jina la "Muungano wa Matumaini" au "Amani ya Hormuz". 

Rais Rouhani akihutubia Baraza Kuu la UN

Miongoni mwa malengo makuu ya pendekezo hilo ni kuimarisha mshikamano, maelewano na uhusiano mwema, kustawisha ushirikiano baina ya nchi za Ghuba ya Uajemi, kuheshimu mamlaka ya kujitawala na mipaka ya ardhi ya nchi hizo, kupambana na ugaidi na misimamo mikali, kudhamini usalama wa nishati na safari za meli na kadhalika.