Nov 17, 2019 08:15 UTC
  • Raisi: Uislamu ndio unaolinda haki za binadamu, si Wamagharibi

Mkuu wa Vyombo vya Mahakama vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekosoa dhana kuwa nchi za Magharibi ndio walinzi wa haki za binadamu na kueleza bayana kuwa, Uislamu ndio umelinda na kuheshimu kikamilifu haki za binadamu.

Sayyid Ibrahim Raisi alisema hayo jana Jumamosi katika hotuba yake aliyoitoa kileleni mwa Kongamano la 33 la Kimataifa la Umoja wa Kiislamu hapa nchini Iran na kuongeza kuwa, "Hii leo, haki za binadamu kwa mujibu wa Uislamu ndizo tu zinazoweza kutoa dhamana ya kuhehimiwa haki hizo." 

Amesema nchi za Magharibi zinazodai kuwa watetezi wa haki za binadamu, ndio wakiukaji wakubwa wa haki hizo. Amesema Uislamu ndio una dalili na hoja za wazi juu ya masuala ya haki za binadamu na ambazo zinatekelezeka.

Kadhalika amezitaka nchi za Kiislamu kuimarisha umoja na mshikamano wao, sambamba na kuboresha uhusiano wao wa kiutamaduni, kijamii na kiuchumi.

Baadhi ya washiriki wa Kongamano la 33 la Kimataifa la Umoja wa Kiislamu

Hii ni katika hali ambayo, Iran imepinga azimio dhidi yake kuhusu haki za binadamu ambalo limetolewa hivi karibuni na Umoja wa Mataifa na kusisitiza kuwa uamuzi huo umetokana na utashi wa kisiasa.

Wizara ya Mamabo ya Nje ya Iran imesema kupasishwa azimio hilo ni mfano wa unafiki na nchi za Magharibi kutumia vibaya mfumo wa Umoja wa Mataifa kulenga nchi huru na zinazojitegemea.

Tags