Spika wa Iran: Utawala wa Kizayuni wa Israel unasambaratika kwa ndani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i61802-spika_wa_iran_utawala_wa_kizayuni_wa_israel_unasambaratika_kwa_ndani
Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amesema kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel umo katika hali ya kusambaratika kutokea ndani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 24, 2020 22:08 UTC
  • Spika wa Iran: Utawala wa Kizayuni wa Israel unasambaratika kwa ndani

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amesema kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel umo katika hali ya kusambaratika kutokea ndani.

Mohammad Baqer Qalibaf ameyasema hayo katika mazungumzo yake na balozi wa Palestina mjini Tehran na kuongeza kuwa, Waziri Mkuu mtendajinai wa Israel yuko katika mgogoro wa ndani kwa miezi kadhaa sasa kwa ajili ya kuunda baraza lake la mawaziri na mgogoro huu ni kielelezo cha kusambaratika kwa ndani utawala huo wa Kizayuni. 

Spika wa Bunge la Iran amesema Palestina ndiyo kadhia nambari moja ya Ulimwengu wa Kiislamu na kuongeza kuwa, himaya na misaada ya Iran kwa malengo na matukufu ya watu wa Palestina inaakisi siasa za kimsingi za Jamhuri ya Kiislamu kuhusiana na Palestina. 

Kwa upande wake balozi wa Palestina mjini Tehran, Salah al Zawawi amesema kuwa baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran hayati Imam Ruhullah Khomeini alitekeleza mpango ambao ulitoa changamoto kwa njama zote za maadui yaani Marekani na Wazayuni. Al Zawawi ameongeza kuwa, baada ya kuaga dunia Imam Khomeini, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei alilipa umuhimu mkubwa suala la ukombozi wa Palestina na umoja baina ya Waislamu.

Balozi wa Palestina mjini Tehran pia ameashiria njama zinazofanywa na Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel kwa ajili ya kuzuia umoja na mshikamano kati ya nchi za Kiislamu na akasisitiza kuwa, kuangamia dola haramu la Israel ni jambo lisilo na chembe ya shaka.