SEPAH: Vikwazo vya silaha haviwezi kuathiri hali ya ulinzi ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i61860-sepah_vikwazo_vya_silaha_haviwezi_kuathiri_hali_ya_ulinzi_ya_iran
Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH amesisitiza kuwa, vikwazo vya silaha vya adui havina taathira yoyote katika hali ya ulinzi nchini Iran na kuongeza kuwa, mifumo yote ya silaha ya jeshi la nchi kavu la SEPAH imefikia katika hatua ya kujitosheleza kikamilifu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 27, 2020 07:13 UTC
  • SEPAH: Vikwazo vya silaha haviwezi kuathiri hali ya ulinzi ya Iran

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH amesisitiza kuwa, vikwazo vya silaha vya adui havina taathira yoyote katika hali ya ulinzi nchini Iran na kuongeza kuwa, mifumo yote ya silaha ya jeshi la nchi kavu la SEPAH imefikia katika hatua ya kujitosheleza kikamilifu.

Ikumbukwe kuwa, kadiri muda wa utekelezaji wa kipengee cha kuiondolea Iran vikwazo vya silaha kwa mujibu wa azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa unavyokaribia, ndivyo Marekani inavyozidisha mashinikizo yake ya kuzuia kutekelezwa azimio hilo lililopasisha makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.

Meja Jenerali Hossein Salami, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH amesema leo Jumamosi wakati alipokagua maonyesho ya mafanikio ya Taasisi ya Utafiti na Jihadi ya Kujitosheleza ya Jeshi la Nchi Kavu la SEPAH hapa Tehran kuwa, mashinikizo na vikwazo vya kidhalimu vya maadui dhidi ya Mapinduzi ya Kiislamu na Taifa la Iran hasa katika upande wa silaha yametoa fursa nzuri ya kujiimarisha vilivyo kiulinzi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Miongozi mwa vifaru vya kisasa vilivyotengenezwa na vijana wenye ghera wa Iran

 

Amesema: Silaha zote nyepesi na nzito, za deraya na mizinga na makombora, shughuli zote za uhandisi na ufundi, mifumo ya kukusanya taarifa za kiinelijinsia na rada za kila namna zinazoimarisha ulinzi nchini Iran zimetengenezwa na vijana wenye ghera wa Iran.

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH aidha amegusia nia ya jeshi hilo ya kuzinduwa mifumo ya kisasa kabisa na ya kustaajabisha ya kiulinzi humu nchini karibuni hivi na kusisitiza kuwa, Jeshi la Nchi Kavu la SEPAH limejizatiti vilivyo kwa silaha zake lenyewe na za kisasa ili lisibaki nyuma katika teknolojia zinazozidi kupiga hatua siku baada ya siku duniani.