Aug 28, 2020 12:35 UTC
  • Iran: 'Mashariki ya Kati' mpya itaanzishwa kwa kutimuliwa Marekani katika eneo

Msaidizi maalumu wa Spika wa Bunge la Iran katika masuala ya kimataifa amesema: 'Mashariki ya Kati' mpya itaundwa baada ya kuhakikisha Marekani imeshatimuliwa kikamilifu katika eneo hili la Asia Magharibi.

Hossein Amir-Abdollahian, msaidizi maalumu wa Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu katika masuala ya kimataifa ameyasema hayo katika ujumbe aliotuma kwenye ukurasa wa kijamii wa Twitter kumjibu Brian Hook, aliyekuwa mwakilishi wa rais wa Marekani katika masuala ya Iran aliyedai kwamba kuanzishwa uhusiano kati ya Imarati na Israel ni kujengwa kwa Mashariki ya Kati mpya.

Abdollahian amesema: Watawala wa White House inawapasa wajue kwamba Mashariki ya Kati mpya itajengwa kwa kuhakikisha Marekani imetimuliwa kikamilifu katika eneo hili. 

Hossein Amir-Abdollahian amebainisha kuwa Mashariki ya Kati mpya ni eneo lisilo wakamaji wowote wa maziwa wa Kimarekani.

Bin Zayed na Netanyahu

Kufuatia hatua kadhaa zilizochukuliwa na Rais Donald Trump wa Marekani kwa lengo la kurahisisha uanzishwaji uhusiano wa kawaida kati ya Imarati na utawala haramu wa Kizayuni, tarehe 13 Agosti pande hizo mbili za Abu Dhabi na Tel Aviv zilisaini mkataba na kuafikiana rasmi kuanzisha uhusiano kamili wa kidiplomasia.

Katika miaka ya karibuni, viongozi wa Saudi Arabia na Imarati wamechukua hatua nyingi kwa ajili ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel, hatua ambazo kasi yake iliongezeka zaidi baada ya Donald Trump kuingia madarakani nchini Marekani mnamo mwaka 2016.../

Tags