Balozi wa Iran UN: Vikwazo vya Marekani ni jinai dhidi ya binadamu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i63589-balozi_wa_iran_un_vikwazo_vya_marekani_ni_jinai_dhidi_ya_binadamu
Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa iliyoko mjini Geneva Uswisi amesema vikwazo vya upande mmoja vya Marekani dhidi ya Iran ni jinai dhidi ya binadamu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 23, 2020 03:49 UTC
  • Balozi wa Iran UN: Vikwazo vya Marekani ni jinai dhidi ya binadamu

Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa iliyoko mjini Geneva Uswisi amesema vikwazo vya upande mmoja vya Marekani dhidi ya Iran ni jinai dhidi ya binadamu.

Esmaeil Baghaei Hamaneh amesema hayo leo katika mkutano wa kawaida wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa na kuongeza kuwa, hatua ya Ulaya ya kutoichukulia Washington hatua ya kivitendo mkabala wa vikwazo vyake hivyo haikubaliki.

Hamaneh ameeleza bayana kuwa, jamii ya kimataifa ina wajibu wa kushikamana na kupinga vitendo hivi vya mabavu na vya kidhalimu vya Marekani.

Mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya juu wa Iran amesema wanaotangaza na kutekeleza vikwazo hivyo vya kidhalimu wanapaswa kubebeshwa dhima na jamii ya kimataifa.

Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa iliyoko mjini Geneva, Uswisi amebainisha kuwa, mfano hai wa kuthibitisha ubeberu wa Marekani kwa dunia ni madai yake ya hivi karibuni kuwa imevirejesha vikwazo vya Baraza la Usalama la UN dhidi ya Iran licha ya pingamizi kutoka kwa wanachama wa taasisi hiyo kubwa zaidi ya UN na Umoja wa Ulaya.

Vikwazo vya US hata katika janga la corona linaloisumbua dunia

Amesema kimya cha jamii ya kimataifa mkabala wa ubabe huo wa Marekani kimeifanya Washington isizisaze hata taasisi za kimataifa kama vile Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC), katika uraibu wake wa kuwekeana vikwazo.

Mwakilishi huyo wa Iran katika UN amesema Jamhuri ya Kiislamu itaendelea kutekeleza sera yake ya 'muqawama wa kiwango cha juu zaidi' kukabiliana na mashinikizo ya hali ya juu ya Marekani dhidi yake.