Iran: Kuchelewa kutuondolea vikwazo ni kwa maslahi ya mradi wetu wa nyuklia
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i68874-iran_kuchelewa_kutuondolea_vikwazo_ni_kwa_maslahi_ya_mradi_wetu_wa_nyuklia
Msemaji wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran amesema kuchelewesha kuliondolea taifa hili vikwazo ni kwa maslahi ya mradi wa nyuklia wenye malengo ya amani wa Jamhuri ya Kiislamu.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Apr 10, 2021 03:33 UTC
  • Iran: Kuchelewa kutuondolea vikwazo ni kwa maslahi ya mradi wetu wa nyuklia

Msemaji wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran amesema kuchelewesha kuliondolea taifa hili vikwazo ni kwa maslahi ya mradi wa nyuklia wenye malengo ya amani wa Jamhuri ya Kiislamu.

Behrouz Kamalvandi ameashiria mkutano wa Vienna wa Kamisheni ya Pamoja ya makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na kusema kuwa, "sisi tunasonga mbele katika uga wa nyuklia, na iwapo hakuna chochote kitachofanyika katika kuiondolea Iran vikwazo, tutapiga hatua kubwa ya kiufundi na hali yetu itakuwa bora zaidi kadiri siku zinavyopita."

Amesisitiza kuwa, jambo muhimu kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika vikao vya Vienna ni kuondolewa vikwazo 1,600 ilivyowekewa Iran na utawala uliopita wa Marekani wa rais Donald Trump.

Mkutano wa Kamisheni ya Pamoja ya JCPOA mjini Vienna

Kamalvandi ameeleza bayana kuwa, Iran haitapoteza chochote kwa kuchelewa kuondolewa vikwazo kwani idadi ya mashinepewa (centrifuge) na mashine nyinginezo za kisasa za nyuklia za Iran inaendelea kuongezeka siku baada ya siku.

Msemaji wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran ameongeza kuwa, kamati za vikwazo na ufundi za Kamisheni ya Pamoja ya JCPOA zinatazamiwa kukutana tena Jumatano kujadili kwa kina vikwazo haramu dhidi ya Iran.