Iran yazindua mafanikio 133 katika Siku ya Kitaifa ya Teknolojia ya Nyuklia
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i68882-iran_yazindua_mafanikio_133_katika_siku_ya_kitaifa_ya_teknolojia_ya_nyuklia
Mafanikio 133 ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika uga wa teknolojia ya nyuklia yamezinduliwa leo katika sherehe maalumu zilizofanyika kwa njia ya video kwa mnasaba wa Siku ya Kitaifa ya Teknolojia ya Nyuklia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 10, 2021 08:01 UTC
  • Iran yazindua mafanikio 133 katika Siku ya Kitaifa ya Teknolojia ya Nyuklia

Mafanikio 133 ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika uga wa teknolojia ya nyuklia yamezinduliwa leo katika sherehe maalumu zilizofanyika kwa njia ya video kwa mnasaba wa Siku ya Kitaifa ya Teknolojia ya Nyuklia.

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameongeza sherehe hizo zilizofanyika kwa njia ya video za uzinduzi wa miradi mikubwa ya nyuklia ya Iran katika mikoa ya Tehran, Markazi, Isfahan, Alborz na Qom.

Akizungumza leo Jumamosi, Mkuu wa Shirika la Atomiki la Iran, Ali Akbar Salehi amesema Jamhuri ya Kiislamu inataka kupanua shughuli zake za nishati ya nyuklia kwa kufuata miongozo na sheria za kimataifa.

Dakta Salehi amesema wanasayansi na wahandisi Wairani wamefanikiwa na kupiga hatua kubwa katika uga wa nyuklia licha ya vizingiti na vikwazo shadidi vya maadui.

Ali Akbar Salehi

Salehi amebainisha kuwa, baadhi ya mafanikio hayo ni katika sekta mbalimbali kama vile uzalishaji wa mashinepewa au centrifuge zinazohitajika katika vituo vya kuchangia damu, tiba na tanuri nyuklia. 

Naye Behrouz Kamalvandi, Msemaji wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu haitapoteza chochote kwa kuchelewa kuondolewa vikwazo kwani idadi ya mashinepewa (centrifuge) na mashine nyinginezo za kisasa za nyuklia za Iran inaendelea kuongezeka siku baada ya siku.