Ali Akbar Velayati: Israel inafanya njama za kuzigawa nchi za Kiislamu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i70-ali_akbar_velayati_israel_inafanya_njama_za_kuzigawa_nchi_za_kiislamu
Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya kimataifa amesema kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel unafanya njama za kuzigawa nchi za Kiislamu, lakini licha ya njama hizo katu hautafanikiwa kufikia malengo yake.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 27, 2016 10:07 UTC
  • Ali Akbar Velayati: Israel inafanya njama za kuzigawa nchi za Kiislamu

Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya kimataifa amesema kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel unafanya njama za kuzigawa nchi za Kiislamu, lakini licha ya njama hizo katu hautafanikiwa kufikia malengo yake.

Ali Akbar Velayati ambaye pia ni Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Kiistratijia cha Halamashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kwamba, siasa za utawala wa Kizayuni wa Israel ni kuzigawa nchi za Kiislamu katika Mashariki ya Kati na ndio maana umekuwa ukizusha fitina na mifarakano baina ya nchi za Kiislamu. Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Kiistratijia cha Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ameashiria pia matamshi ya Waziri wa Sheria wa Israel juu ya ulazima wa kuasisiwa dola la Kikurdi baina ya Iran na Uturuki na kusema kwamba, hakuna wakati ambao utawala huo ghasibu utafanikiwa kufikia malengo yake hayo. Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya kimataifa aidha amesema kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel unataka kuasisi Israel ya pili na hata ya tatu katika Mashariki ya Kati na kwamba, Uturuki ikiwa nchi muhimu katika Ulimwengu wa Kiislamu haitoruhusu mabeberu na Wazayuni kufikia malengo yao ya kuzigawanya nchi za Kiislamu.