Rais Rouhani: Njia pekee ya kukabiliana na wavamizi ni mapambano
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i70552-rais_rouhani_njia_pekee_ya_kukabiliana_na_wavamizi_ni_mapambano
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, njia pekee ya kukabiliana na wavamizi, ni mapambano.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
May 25, 2021 22:19 UTC
  • Rais Rouhani: Njia pekee ya kukabiliana na wavamizi ni mapambano

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, njia pekee ya kukabiliana na wavamizi, ni mapambano.

Rais wa Iran ameyasema hayo Jumanne katika ujumbe ambao amemtumia mwenzake wa Lebanon Michel Aoun kwa mnasaba wa ushindi wa taifa la Lebanon dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel mwaka 2000

Amesema kukombolwa maeneo ya kusini mwa Lebanon ambayo yalikuwa yanakaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel miaka 21 iliyopita ni ushindi uliojaa fakhari kwa taifa la Lebanon.

Rouhani amesema ushindi huo ulionyesha wazi kuwa njia pekee ya kukabiliana na wavamizi ni mataifa kusimama kidete na kupambana.

Rais Rouhani halikadhalika amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inafungamana na taifa na serikali ya Lebanon katika kulinda umoja na mipaka ya nchi hiyo.

 

Michel Aoun

Kila mwaka mwezi 25 Mei, Lebanon huadhimisha kumbukumbu ya kuondoka kwa  madhila wanajeshi vamizi wa Isrel katika ardhi zake za kusini. Siku hii nchini Lebanon hujulikana kama Siku ya Kitaifa ya Mapambano na Ukombozi.