Jun 15, 2021 10:58 UTC
  • Rais Rouhani: Vikwazo na vita vya kiuchumi vitambuliwe kuwa ni jinai za kimya kimya

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, vikwazo na vita vya kiuchumi lazima vipewe jina la jinai ya kimya kimya dhidi ya binadamu duniani.

Rais Hassan Rouhani amesema hayo katika kikao cha leo cha Kamati ya Uratibu wa Kiuchumi ya Serikali na kuongeza kuwa, kuna wajibu wa kutangazwa kwa walimwengu wote kwamba jinai za vita vya kiuchumi na walioweka vikwazo hivyo vya pande zote ambavyo havijawahi kuwekewa taifa lolote duniani isipokuwa Iran, wote wahesabiwe kuwa ni watenda jinai dhidi ya binadamu. Serikali ya Donald Trump ya Marekani na kila aliyechangia katika vikwazo vya kiwango cha juu kupindukia dhidi ya wananchi wa Iran, lazima wahesabiwe na walimwengu kuwa ni watenda jinai dhidi ya binadamu.

Taifa la Iran limesambaratisha vikwazo vya Marekani

 

Amegusia pia madhara ya vita vya kiuchumi katika ustawi wa nchi na maisha ya watu wa kawaida na kuongeza kuwa, kwa kawaida jinai dhidi ya binadamu inayotambuliwa na watu wengi duniani ni ile inayofanyika kwenye vita na mapigano ya kijeshi, wakati ambapo vikwazo na vita vya kiuchumi pia ni lazima vihesabiwe kuwa ni jinai dhidi ya binadamu zinazofanyika kimya kimya.

Katika sehemu nyingine ya matamshi yake, Rais Rouhani amesema, kuna wajibu pia wa kutambulishwa kwa walimwenu  hati ya muqawama na uendeshaji wa mapambano wa taifa la Iran katika vita vya kiuchumi, sambamba na kuoneshwa walimwengu hati ya jinai za rais wa zamani wa Marekani Donald Trump ambaye aliliwekea vizuizi na vikwazo vingi taifa la Iran ili lishindwe kuendelea na kustawi na pia wananchi wake wapate tabu katika maisha yao bali hata katika masuala ya afya na matibabu.

Tags