Rais wa Croatia alakiwa rasmi na Rais Rouhani
Rais Hassan Rouhani amemlaki rasmi Rais Kolinda Grabar-Kitarović wa Croatia katika jengo la kihistoria na kiutamaduni la Ikulu ya Saad Abad mjini Tehran.
Alipowasili jana jioni, Bi Kitarović ambaye amefanya safari rasmi ya siku tatu nchini kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alilakiwa na Waziri wa Viwanda, Madini na Biashara Mohammad Reza Neematzadeh.
Baada ya hafla ya kulakiwa rasmi, marais wa Iran na Croatia walianza mazungumzo ya pande mbili yaliyoshirikisha pia jumbe za ngazi za juu za nchi zao.
Hati kadhaa za maelewano na ushirikiano zinatazamiwa kusainiwa katika safari hiyo ya Rais wa Croatia hapa nchini.
Katika safari yake hiyo Bi Kolinda Grabar-Kitarović ameandamana na ujumbe wa ngazi za ju wa kiuchumi na wamiliki wa mashirika na makampuni ya biashara na viwanda wa nchi yake. Akiwa hapa nchini, Rais wa Croatia anatazamiwa pia kushiriki katika kikao cha pamoja cha wawakilishi wa sekta za uchumi na za binafsi wa nchi mbili.../