Baqeri: Marekani imeondoka Afghanistan baada ya kushindwa kwa fedheha
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i74044-baqeri_marekani_imeondoka_afghanistan_baada_ya_kushindwa_kwa_fedheha
Mkuu wa Kamandi ya Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, Marekani imeondoka nchini Afghanistan baada ya kushindwa kwa fedheha.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Aug 29, 2021 07:39 UTC
  • Baqeri: Marekani imeondoka Afghanistan baada ya kushindwa kwa fedheha

Mkuu wa Kamandi ya Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, Marekani imeondoka nchini Afghanistan baada ya kushindwa kwa fedheha.

Meja Jenerali Mohammad Baqeri, Mkuu wa Kamandi ya Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran akizungumza leo mjini Tehran wakati wa kumuarifisha waziri mpya wa ulinzi Jenerali Mohammad Reza Ashtiani na kumuenzi waziri anayeondoka Brigedia Jenerali Amir Hatami amesema: "Jinai ya mwisho ya Marekani nchini Afghanistan ni kuwa ilitumia dola bilioni mbili kwa ajli ya Jeshi la Afghanistan na kulibadilisha kuwa jeshi lisilo na uwezo.

Mkuu wa Kamandi ya Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran  ameashiria pia jinai za Marekani na hujuma zake kadhaa za kijeshi katika eneo la Asia Magharibi na kuongeza kuwa, njama zaidi zinaonekana zikiendelezwa na Marekani katika maeneo mbali mbali na hivyo katika mazingra kama hayo, ni jambo la dharura kwa Iran kuimarisha uwezo wake wa kujihami kwa kutegemea uwezo wa ndani ya nchi.

Makombora ya kujihami ya Iran

Meja Jenerali Baqeri amesema muundo wa vita umebadilika na kuongeza kuwa: "Vita vya leo na mustakabali vitashabihiana kidogo tu na vita vya miaka ya nyuma. Vita vya mwaka  jana vya Nagorno-Karabakh havikushabihiana na vita vya miaka ya nyuma kwani katika vita hivyo kulitumika teknolojia mpya."

Aidha amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iko katika eneo nyeti kijiografia duniani ambalo linakumbwa na misukosuko mingi na kuongeza kuwa, wizara ya ulinzi ina jukumu la kuunda zana na silaha kwa kuzingatia mabadiliko ya sasa na ya baadaye katika medani za vita.