Iran imejitosheleza kuzalisha dawa za kukabiliana na COVID-19
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i76694-iran_imejitosheleza_kuzalisha_dawa_za_kukabiliana_na_covid_19
Waziri wa Afya wa Iran amesema nchi hii sasa imejitosheleza kikamilifu katika kuzalisha dawa za kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19.
(last modified 2026-03-17T04:36:21+00:00 )
Nov 08, 2021 22:59 UTC
  • Iran imejitosheleza kuzalisha dawa za kukabiliana na COVID-19

Waziri wa Afya wa Iran amesema nchi hii sasa imejitosheleza kikamilifu katika kuzalisha dawa za kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19.

Daktar Bahraim Eynollahi ameyasema hayo Jumatatu wakati alipokuwa akizungumza na waandishi habari na kuongeza kuwa, vituo vitano vimepata idhini kuzalisha chanjo ya  COVID-19 zikiwemo Barakat, Fakhra na Razi huku akielezea matumaini kuwa  dozi ya tatu ya chanjo ya COVID-19 itakuwa ni ile  iliyozalishwa nchini.

Dakta Eynollahi  aidha amesema, hadi sasa dozi milioni 150 za chanjo ya COVID-19 zimeingizwa nchini na hadi sasa watu nchini Iran wamepokea dozi milioni 95.

Halikadhalika Waziri wa Afya nchini Iran amesema,  Iran imevunja rekodi ya kutoa chanjo ya COVID 19 kutokana na jitihada za usiku na mchana za wafanyakazi wa sekta ya afya. Katika rekodi hiyo ya dunia Iran imedunga dozi milioni moja na laki sita hamisini elkfu kwa siku na kwa wiki watu milioni nane wamepata dozi ya chanjo hiyo ya COVID-19.

Chanjo ya Barakat ya Iran

Iran iko mbioni kuunda chanjo kadhaa za COVID-19,  na hivi sasa tayari chanjo COVIran Barekat iliyotegenezwa kikamilifu hapa nchini inatumika katika zoezi la chanjo huku ikisubuiri idhini ya Shirika la Afya Duniani ili kuweza kutumiwa kimatiafa.  Chanjo zingine ambazo zimepiga hatua nzuri katika majaribio ni pamoja na Fakhra, Noora  na chanjo ya pamoja ya Taasisi ya Chanjo ya Finlay ya Cuba na Taasisi ya Chanjo ya Pasteur ya Iran.