Iran yazitaka nchi za Kiislamu kupambana na misimamo mikali
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i8659-iran_yazitaka_nchi_za_kiislamu_kupambana_na_misimamo_mikali
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewataka viongozi wa nchi za Kiislamu kushirikiana na kufanya kazi bega kwa bega kwa lengo la kukabiliana na misimamo ya kufurutu ada.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jun 07, 2016 07:24 UTC
  • Iran yazitaka nchi za Kiislamu kupambana na misimamo mikali

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewataka viongozi wa nchi za Kiislamu kushirikiana na kufanya kazi bega kwa bega kwa lengo la kukabiliana na misimamo ya kufurutu ada.

Katika ujumbe wake kwa viongozi wa nchi za Kiislamu kwa mnasaba wa kuwadia mwezi mtukufu wa Ramadhani, Rais Hassan Rouhani amewaasa viongozi wa nchi hizo kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa dunia ni pahala salama kutokana na ghasia, machafuko na misimamo iliyochupa mipaka.

Amesema na hapa tunamnukuu: "Katika kipindi hiki muhimu kwa historia ya Uislamu, taswira ya kuogofya na bandia ya Uislamu inatishia turathi za kihistoria, falsafa na udugu wa wafuasi wa dini hii tukufu." Mwisho wa kunukuu.

Rais Hassan Rouhani amesisitiza kuwa, kuna haja kwa Waislamu wote kutambulisha picha halisi na sahihi ya Uislamu na kuudhihirishia ulimwengu kuwa Uislamu ni dini ya amani, huruma na inayohimiza ushirikiano na mshikamano. Rais Rouhani ametamatisha ujumbe wake kwa nchi za Kiislamu kwa mnasaba wa kuwadia mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kusema kuwa, mwezi huu mtukufu unatoa fursa na kipindi cha kuunga na kuimarisha udugu miongoni mwa Waislamu, huku akitoa mkono wa kheri na fanaka kwa viongozi wa nchi za Kiislamu, serikali na wananchi kwa ujumla.