Rais Rouhani awasili Paris akiwa katika ziara zake za Ulaya
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i88-rais_rouhani_awasili_paris_akiwa_katika_ziara_zake_za_ulaya
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo alasiri kwa wakati wa Ufaransa amewasili Paris mji mkuu wa nchi hiyo akiwa katika marhala ya pili ya ziara zake za Ulaya.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 27, 2016 12:59 UTC
  • Rais Rouhani awasili Paris akiwa katika ziara zake za Ulaya

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo alasiri kwa wakati wa Ufaransa amewasili Paris mji mkuu wa nchi hiyo akiwa katika marhala ya pili ya ziara zake za Ulaya.

Safari ya Rais Hassan Rouhani wa Iran huko Ufaransa imefanyika kufuatia mwaliko wa rasmi wa Rais Francois Hollande wa nchi hiyo. Rais wa Iran amesema mbele ya waandishi wa habari baada ya kuwasili Paris kuwa ziara yake nchini humo ni hatua muhimu katika kuimarisha uhusiano kati ya Iran na Ufaransa na kusisitiza kuhusu kuimarisha uhusiano kati ya Iran na Umoja wa Ulaya ikiwemo Ufaransa.

Rais Rouhani amesema, Iran inataka kuimarisha uhusiano na Ufaransa katika fremu ya maslahi ya nchi mbili.

Rais Rouhani leo usiku atashiriki kikao cha pamoja cha wanaharakati wa masuala ya kiuchumi na wafanyabishara wa Ufaransa na Iran na baada ya hapo atakuwa na mazungumzo na Spika wa Seneti ya Ufaransa.