Kan'ani: Haki za binadamu ni mchezo wa nchi kadhaa za wahalifu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i91250-kan'ani_haki_za_binadamu_ni_mchezo_wa_nchi_kadhaa_za_wahalifu
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Nasser Kan'ani, ametaja mauaji ya kijana wa Kipalestina kwa kupigwa risasi moja kwa moja na askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel kuwa yanastahili jibu la kimataifa na kusema: "Haki za binadamu zimekuwa mchezo wa nchi kadhaa za kihalifu."
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Dec 03, 2022 03:04 UTC
  • Kan'ani: Haki za binadamu ni mchezo wa nchi kadhaa za wahalifu

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Nasser Kan'ani, ametaja mauaji ya kijana wa Kipalestina kwa kupigwa risasi moja kwa moja na askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel kuwa yanastahili jibu la kimataifa na kusema: "Haki za binadamu zimekuwa mchezo wa nchi kadhaa za kihalifu."

Nasser Kan'ani ameyasema hayo katika ujumbe wake wa Twitter na kuandika kuwa: Kuuliwa shahidi kijana wa Kipalestina, Ammar Hamdi Muflih, 22, kwa kupigwa risasi kadhaa za moja kwa moja za mwajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel tena kadamnasi kunastahili jibu la kimataifa. Jinai za kila siku za utawala mtenda jinai wa Israel hazilaaniwi na wale wanaodai kutetea haki za binadamu, wala hakuna kamati ya kutafuta ukweli iliyoundwa kwa ajili ya kufuatilia uhalifu huo! Ameongeza kuwa: Haki za binadamu zimekuwa mchezo wa madola ya watenda jinai. 

Kijana wa Kipalestina, Ammar Hamdi Muflih, aliuawa shahidi kwa kupigwa risasi na askari wa Israel alasiri ya jana Ijumaa katika kitongoji cha Hawara huko kusini mwa eneo la Nablus.

Katika kipindi cha miezi michache iliyopita mashambulizi ya jeshi la utawala wa Kizayuni yameongezeka kwenye maeneo mbalimbali ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan hususan Jenin na Nablus, na makumi ya Wapalestina wameuawa shahidi na mamia ya wengine kujeruhiwa katika mashambulizi hayo.