Amir- Abdollahian: Dunia inakumbwa na migogoro ya matabaka mengi na tata
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i92836-amir_abdollahian_dunia_inakumbwa_na_migogoro_ya_matabaka_mengi_na_tata
Akizungumza mkutano kwa njia ya mtandao wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa "Sauti ya Kusini",Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameeleza mitazamo na rai za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusiana na masuala muhimu ya kimataifa na nafasi yenye taathira ya nchi za Kusini katika uga wa kimataifa.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jan 13, 2023 07:36 UTC
  • Amir- Abdollahian: Dunia inakumbwa na migogoro ya matabaka mengi na tata

Akizungumza mkutano kwa njia ya mtandao wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa "Sauti ya Kusini",Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameeleza mitazamo na rai za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusiana na masuala muhimu ya kimataifa na nafasi yenye taathira ya nchi za Kusini katika uga wa kimataifa.

Hossein Amir-Abdollahian alisisitiza jana katika mkutano huo kwamba: dunia sasa inakumbwa na migogoro ya matabaka mengi na tata; na huku ikitaraji kurejea kwa ugonjwa wa Uviko-19, dunia inaendelea kutatizwa na vita dhidi ya ugaidi,  umaskini, taathira mbaya za ufakiri ,kukosekana uadilifu wa kiuchumi sambamba na kuporomoka hali ya uchumi na mfumuko wa bei. 

Amir- Abdollahian ameongeza kuwa, pande za kimataifa badala ya kufikiria kushirikiana ili kutatua matatizo yanayoisibu dunia na kupatia ufumbuzi migogoro mbalimbali;zinafanya juhudi kwa maslahi yazo ya upande mmoja; na zinatoa mashinikizo na kuzikandamiza nchi huru duniani na zile zinazotaka kuwepo kambi za pande kadhaa kwa kutumia ushawishi walionao katika taasisi za kifedha na za kiuchumi za kimataifa na kupitia kuzitwisha nchi nyingine vikwazo vya upande moja na vya kidhulma.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran wakati huo huo amesisitiza kuwa, hatua za kivitendo zimechukuliwa kwa lengo la kuboresha amani, uthabiti na usalama wa kimataifa na kutangaza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iko tayari kushirikiana na kundi la G-20. 

Katika mkutano huo wa mawaziri wa Mambo ya Nje wa wa "Sauti ya Kusini", Mawaziri wa Mambo ya Nje wa India, Armenia, Oman, Maldive, Panama, Jamaica, Kenya, El Salvador, Georgia, Uganda, Tunisia na Jamhuri ya Dominica wamebadilishana mawazo na kubainisha fikra na mitazamo yao mbalimbali.