Iran na Iraq zatiliana saini makubaliano ya kuimarisha usalama mipakani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i95310-iran_na_iraq_zatiliana_saini_makubaliano_ya_kuimarisha_usalama_mipakani
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Iraq zimetiliana sainii makubaliano ya kuimarisha usalama wa mipakani hatua ambayo maafisa wa Baghdad wanasema inalenga hasa kuimarisha usalama wa mpakani na eneo la Kurdistan ya Iraq, ambapo Tehran inasema, makundi yenye silaha yamekuwa tishio kwa usalama wake.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 20, 2023 03:32 UTC
  • Iran na Iraq zatiliana saini makubaliano ya kuimarisha usalama mipakani

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Iraq zimetiliana sainii makubaliano ya kuimarisha usalama wa mipakani hatua ambayo maafisa wa Baghdad wanasema inalenga hasa kuimarisha usalama wa mpakani na eneo la Kurdistan ya Iraq, ambapo Tehran inasema, makundi yenye silaha yamekuwa tishio kwa usalama wake.

Makubaliano hayo yametiwa saini mjini Baghdad kati ya Ali Shamkhani Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran na Qassim al-A'raji, mshauri wa usalama wa taifa wa Iraq kwa usimamizi wa Waziri Mkuu wa Iraq Mohammed Shia al-Sudani.

Taarifa iliyotolewa ofisi ya Waziri Mkuu wa Iraq imeeleza kuwa, makubaliano ya pamoja ya usalama ya yaliyotowa saini jana Jumapili yanajumuisha uratibu katika "kulinda mipaka ya pamoja kati ya nchi hizo mbili sambamba na kuunganisha ushirikiano katika nyanja kadhaa za usalama".

Chini ya makubaliano hayo ya usalama Iraq imeahidi kwamba haitaruhusu makundi yenye silaha kutumia adhi yake katika eneo la Kurdistan Iraq kufanya mashambulizi yoyote ya kuvuka mpaka dhidi ya jirani yake Iran.

Mazungumzo ya Ali Shamkhani Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran na Waziri Mkuu wa Iraq

 

Ali Shamkhani Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema katika mazungumzo yake na Waziri Mkuu wa Iraq kwamba, ushirikiano wa kimkakati wa Tehran na Baghdad unadhamini amani na ustawi wa eneo hili.

Kwa upande wake Mohammed Shia al-Sudani amesema kkuwa, serikali na taifa la Iraq daima limekuwa likithamini uungaji mkono na msaada wa ndugu zao wa Iran hususan katika nyakati ngumu.

Kadhalikka amesema, mashahidi wa Qassim Soleimani na Abu Mahdi Al-Muhandis ni mfano mwingine wa mataifa mawili ya Iran na Iraq kuwa pamoja.