Kan'ani: Ujumbe wa Nowruz wa Biden kwa Wairani ni uongo mtupu
-
Nasser Kan'ani
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amejibu ujumbe wa Nowruz wa Rais wa Marekani, Joe Biden, na kusema ujumbe huo ni madai ya uongo.
Nasser Kan'ani ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba: Uadui Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu na taifa la Iran ni sehemu isiyobadilika ya siasa za nje za utawala wa Marekani.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema hayo akijibu ujumbe wa eti salamu za Nowruz ambazo hutolewa kila mwaka na viongozi wa Marekani kwa mnasaba wa kuanza mwaka mpya wa Kiirani wa Hijria Shamsia.
Amesisitiza kuwa kufanya uhasama na uadui dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni sehemu isiyobadilika na thabiti katika siasa na sera za kigeni za Marekani.
Kan'ani ameendelea kuandika kuwa: Madai ya uongo ya kuwatetea wanawake wa Kiirani na wakati huo huo kudumisha na kuzididisha vikwazo vya kikatili dhidi ya taifa la Iran ni onyesho la unafiki na uadui wa utawala wa Marekani na viongozi wake wenye chuki dhidi ya Iran.
Wakati huo huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, Nowruz ni sherehe ya urithi wa kiutamaduni, utajiri wa kuwepo wanaadamu wa aina tofauti na fursa ya mazungumzo na mshikamano.
Antonio Guterres amesema hayo katika ujumbe wake wa heri ya mwaka mpya wa Nowruz na kuongeza kuwa: Nowruz ni fursa kwa watu wote kujifunza maadili ya amani, mazungumzo na mshikamano, kuthibitisha mshikamano wa wanadamu na haki za binadamu na utu, kueneza hali ya kuheshimiana na maridhiano, na kulinda sayari ya dunia kwa kwenda sambamba na maumbile ya dunia.
mwakka mpya wa Kiirani wa Hijria Shamsia umeeanza leo nchini Iran na katika nchi na mataifa yote yanayosherehekea Nowruz.