Hatibu wa Swala ya Ijumaa Tehran: Marekani inataka kuangamzia Uislamu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i95472-hatibu_wa_swala_ya_ijumaa_tehran_marekani_inataka_kuangamzia_uislamu
Hatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amezungumzia njama zinazofanywa na Marekani kwa shabaha ya kuuangamiza Uislamu na Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran na kusema kuwa, Marekani daima inafanya mikakati ya kujaribu kupenya kwenye imani na fikra za watu kupitia njia za kipropaganda.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 24, 2023 10:14 UTC
  • Hujjatul-Islam Walmuslimin Kazem Seddiqi
    Hujjatul-Islam Walmuslimin Kazem Seddiqi

Hatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amezungumzia njama zinazofanywa na Marekani kwa shabaha ya kuuangamiza Uislamu na Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran na kusema kuwa, Marekani daima inafanya mikakati ya kujaribu kupenya kwenye imani na fikra za watu kupitia njia za kipropaganda.

Hujjatul-Islam Walmuslimin Kazem Seddiqi ameyasema hayo katika hotuba za Swala ya Ijumaa mjini Tehran na kuongeza kuwa, tangu mwanzoni mwa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Marekani imeendeleza msururu wa vita, vikwazo, hujuma za kkigaidi, kuibua hitilafu za kikaumu kuvuruga usalama kupitia makundi ya wanafiki na kuanzisha fitina na ghasia za aina mbalimbali nchini Iran kwa kadiri kwamba, msimu wa mapukutiko uliopita ilianzisha vita mseto kwa kushirikiana na nchi nyingine za kibeberu ili kuuondoa madarakani utawala wa Kiislamu hapa nchini. 

Hatibu wa Swala ya Ijumaa ya mjini Tehran ameongeza kuwa, katika maandalizi yake ya kutaka kuyaangusha Mapinduzi ya Kiislamu, Marekani ilitayarisha zana za kipropaganda ili kupenya na kuingia katika imani na maarifa ya wananchi na kuharibu moyo wa imani, kujiamini na kujitegemea kwa watu wa Iran.

Swala ya Ijumaa Tehran

Hujjatul-Islam Seddiqi amesisitiza kuwa, Iran imepiga hatua kubwa katika miaka 44 iliyopita licha ya kuwekewa vikwazo eti vya kulemaza, mauaji na hujuma za aina mbalimbali za kigaidi.

Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya mjini Tehran ameeleza kuwa, licha ya mashinikizo ya nje na vita mseto, Serikali ya Awamu ya 13 ya Iran imepata mafanikio makubwa kutokana na uungaji mkono na utambuzi wa wananchi.