Kitengo cha Kimataifa cha Maonyesho ya Qur’ani ya Tehran kuzinduliwa leo
Kitengo cha Kimataifa cha Maonyesho ya 30 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran kinafunguliwa leo Jumatatu, Aprili 3, 2023.
Abdolreza Soltani, mkuu wa kitengo cha kimataifa, amesema kuwa kitengo hicho kitazinduliwa leo Jumatatu kwa kushirikisha Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu, Mohammad Mehdi Esmaeili, na mkuu wa Jumuiya ya Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu (ICRO) Hujjatul-Islam Mohammad Mehdi Imanipour.
Kitengo hicho kitakuwa na msisitizo maalumu katika suala la umoja wa Kiislamu, alisema, akiongeza kuwa nchi shiriki zitaonyesha kazi za sanaa na kutakuwa na warsha.
Amebainisha kuwa wawakilishi kutoka India, Pakistan, Tunisia, Bosnia, Algeria, Indonesia, Malaysia, Tanzania, Kenya na Oman wataonyesha kazi zao za sanaa katika maonyesho hayo.
Zaidi ya hayo, baadhi ya nchi zitawasilisha mafanikio yao ya Qur'ani na kuongeza kuwa mataifa hayo ni pamoja na Russia, Iraq, Algeria, Tunisia, Malaysia, Pakistan, Sri Lanka, Oman, Lebanon na Afghanistan.
Maonyesho ya 30 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran yalifunguliwa rasmi Jumamosi iliyopita na Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Sayyid Ebrahim Raisi.
Maonyesho hayo yalianza katika siku ya 10 ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Kauli mbiu ya maonyesho hayo ambayo yataendelea hadi tarehe 26 ya Mwezi wa Mtukufu wa Ramadhani ni “Ninakusoma” kwa lengo la kuhimiza umuhimu wa kuendelea kusoma Qur’ani Tukufu.