Raisi: Viongozi wa nchi za Kiislamu wafanikishe umoja wa Umma wa Kiislamu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i95856-raisi_viongozi_wa_nchi_za_kiislamu_wafanikishe_umoja_wa_umma_wa_kiislamu
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amemtumia ujumbe Rais wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen akisisitiza umuhimu wa kupatikana umoja wa Umma wa Kiislamu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 03, 2023 08:53 UTC
  • Raisi: Viongozi wa nchi za Kiislamu wafanikishe umoja wa Umma wa Kiislamu

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amemtumia ujumbe Rais wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen akisisitiza umuhimu wa kupatikana umoja wa Umma wa Kiislamu.

Katika ujumbe wake kwa Mehdi Al-Mashat, Rais wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen, Sayyid Ebrahim Raisi, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameitaja Ramadhani kuwa ni mwezi wa ibada, kutakasa nafsi, kujielimisha na kujitenga na mambo ya kidunia, na ameitakia Yemen, Waislamu na wale wote wanaopiga hatua kwenye njia ya haki ustawi na maendeleo.

Katika ujumbe huo, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, viongozi wa nchi za Kiislamu wanapaswa kufanikisha umoja na mshikamano wa Umma wa Kiislamu katika mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kutegemea mafundisho ya Qur'ani Tukufu na kushikamana na masuala ya kiroho na kimaanawi ya mwezi huu wenye kheri na baraka tele.

Raisi amesema kwamba Waislamu wote wanapaswa kuinua juu jina la Uislamu duniani kwa kuchukua hatua na kufanya juhudi za pamoja katika mwelekeo huu.

Uzoefu wa miongo ya hivi karibuni unaonyesha wazi kwamba, maadui siku zote wanafanya mikakati ya kuzuia uhuru na kujitawala halisi kwa Waislamu, na katika muktadha huo wanatumia njia mbalimbali zikiwemo propaganda hasi za vyombo vya habari dhidi ya Waislamu, kuchochea chuki dhidi ya Uislamu, kuwatuhumu Waislamu kuwa na itikadi kali na kwamba ni magaidi na kuibua hitilafu na mgawanyiko miongoni mwa wafuasi wa madhehebu mbalimbali.