Apr 05, 2023 02:37 UTC
  • Maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds kufanyia Aprili 14

Mwenyekiti wa Makao Makuu ya Intifadha na Siku ya Kimataifa ya Quds nchini Iran amesema nara na kaulimbiu ya Siku ya Kimataifa Quds mwaka huu ni: "Palestina ni Mhimili wa Umoja wa Ulimwengu wa Kiislamu, na Quds (Jerusalem) Inakaribia Kukombolewa."

Imam Khomeini MA Mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alitangaza kuwa Ijumaa ya mwisho ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni Siku ya Kimataifa ya Quds.  Waislamu na wapenda haki wamekuwa wakifanya maandamano katika pembe mbalimbali za dunia kila mwaka katika Siku ya Kimataifa ya Quds, na kuonyesha hasira zao dhidi ya siasa za kibaguzi na kikatili zinazotekelezwa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la IRNA, Brigedia Jenerali Ramadhan Shariff Mwenyekiti wa Makao Makuu ya Intifadha na Siku ya Kimataifa ya Quds nchini Iran ameyasema hayo katika kikao cha kuandaa Siku ya Kimataifa ya Quds.

Amesema Siku ya Kimataifa ya Quds mwaka huu itafanyika Ijumaa 23 Ramadhani 1444 Hijria inayosadifiana na 14 Aprili 2023. Amesema Siku ya Kimataifa ya Quds mwaka huu inasadifiana na usiku wa Laylatul Qadr na hivyo hii ni baraka maradufu kwa ulimwengu wa Kiislamu.

Maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds nchini Tanzania katika miaka iliyopita

 

Tags