Amir-Abdollahian: Iran ina wasiwasi na hali inayoshuhudiwa huko Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i96186-amir_abdollahian_iran_ina_wasiwasi_na_hali_inayoshuhudiwa_huko_palestina
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Iran ina wasiwasi na hali ya mambo iinayoshuhudiwa hivi sasa huko Palestina ikiwa ni matokeo ya hatua za kijinai za utawala haramu wa Israel.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 12, 2023 03:37 UTC
  • Amir-Abdollahian: Iran ina wasiwasi na hali inayoshuhudiwa huko Palestina

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Iran ina wasiwasi na hali ya mambo iinayoshuhudiwa hivi sasa huko Palestina ikiwa ni matokeo ya hatua za kijinai za utawala haramu wa Israel.

Hussein Amir-Abdollahian ametuma jumbe tofauti kwa Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Ibrahim Taha, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) wakati huu wa kukaribiana maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds na kubainisha kwamba, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inalaani vitendo vya utumiaji mabavu, ukatili na unyama unaofanywa na utawala vamizi wa Israel dhidi ya taifa la Palestina.

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria katika jumbe zake hizo hatua za kijinai za Israel dhidi ya Palestrina kama mauaji, kutiwa mbaroni watu kiholela, kubomolewa nyumba zao sambamba na kuporwa mali zao na kueleza kwamba, vitendo na hatua hizo zinakinzana wazi kabisa na sheria za kimataifa na haki za binadamu.

Walowezi wa Kizayuni ambao wamekuwa wakivamia mara kwa mara msikiti wa al-Aqswa wakiungwa mkono na kusaidiwa na jeshi la utawala ghasibu wa Israel

 

Kadhalika Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria  utumiaji mbaya wa Israel wa kushughulishwa walimwengu na vita vya Ukraine na kukosoa vikali kimya cha jamii ya kimataifa  sambamba na ubutu wa asasi za kimataifa  sambamba na mataifa yanayodaii kuwa vinara wa kutetea haki za binadamu ulimwenguni.

Amiir-Abdollahian ametoa mwito wa kuchukuliwa hatua za haraka katika Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) na asasi husika za kimataifa katika uga huo ili kuhitimisha madhila na machungu ya wananchi madhulumuu wa Palestina.