Ukurasa mpya wa ushirikiano wa kiuchumi baina ya Iran na Syria
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i96992-ukurasa_mpya_wa_ushirikiano_wa_kiuchumi_baina_ya_iran_na_syria
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran jana Jumatano aliwasili Damascus mji mkuu wa Syria kwa mwaliko rasmi wa rais wa nchi hiyo Bashar al-Assad.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 04, 2023 06:57 UTC
  • Ukurasa mpya wa ushirikiano wa kiuchumi baina ya Iran na Syria

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran jana Jumatano aliwasili Damascus mji mkuu wa Syria kwa mwaliko rasmi wa rais wa nchi hiyo Bashar al-Assad.

Katika safari yake hii Ibrahim Raisi anauongoza ujumbe wa ngazi za juu wa maafisa wa kisiasa na kiuchumi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Sayyid Ibrahim Raisi alisema mjini Damascus hapo jana katika mazungumzo yake na Rais Bashar al-Assa wa nchi hiyo kwamba, hii leo tunaweza kusema kwamba, Syria imevuka matatizo yote ya vikwazo na vitisho na imeibuka na ushindi. Mbali na kuutaja uhusiano wa Syria na Iran kuwa ni wa kidugu, Rais wa Iran alisisitiza kuwa, kama ambavyo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilikuwa pamoja na seriikali ya Syria na wananchi wa nchi hiyo katika vita dhidi ya ugaidi, itakuwa pamoja na serikali na wananchi wa nchi hiyo pia katika kuikarabati na kuijenga tena nchi hiyo.

Katika siku ya kwanza ya safari yake ya siku mbili nchini Syria nchi mbili ziliafikiana na kushirikiana katika fremu ya mpango jumuishi wa kimkakati na wa muda mrefu. Maafiikiano hayo yalifuatiwa na hafla ya kutiliana saini hati 14 za ushirikiano. Baadhi ya nyuga za ushirikiano zilizoafikiwa na pande mbili na kutiliana saini ni nyanja za kibiashara, mafuta, nishati, nyumba, usafiri na uchukuzi, reli, anga, mawasiliano na teknolojia.

Marais wa Iran na Syria baada ya kutiliana saini hati kadhaa za ushirikiano

 

Licha ya kuwa, safari ya Rais Ibrahim Raisi nchini Syria kutokana na kuweko uhusiano imara na madhubuti baina ya nchi hizi, mchango wa mataifa haya mawili yakiwa katika katika mhimili wa muqawama na vilevile matukio ya sasa ya eneo la Asia Magharibi ina umuhimu wa pande kadhaa za kisiasa na kiusalama, lakini moja ya malengo muhimu ya safari hii ni kuongeza kiwango cha ushirikiano wa kiuchumi. Ushahidi wa hilo ni kutiwa saini hati 14 za ushirikiano baina ya pande mbili katika nyuga mbalimbali.

Uchunguzi unaonyesha kuwa, licha ya kuweko ushirikiano imara na madhubuti wa kiusalama na kisiasa baina ya Iran na Syria, lakini ushirikiano wa nchi hizi mbili rafiki katika uga wa kiuchumi hadi sasa umekuwa wa kusuasua. Kwa mfano katika miaka mwili iliyopita usafirishaji wa bidhaa za Iran kuelekea Syria ulikuwa dola milionii 218 mwaka 2021 huku mwaka 2022 ukifikia dola milioni 243. Hii ni katika hali ambayo, baadhi ya mataifa ambayo katika kipindi cha kilele cha mgogoro wa Syria licha ya kwamba, hayakuwa na uhusiano mzuri na nchi hiyo lakini takwimu zinaonyesha kwa, kiwango chao cha ushirikiano wa kibiashara kkilikuwa juu.

 

Filihali Syria imeondokana na jinamizi la ukosefu wa usalama na inashuhudia utulivu wa kiwango fulani. Hata hivyo sekta ya nchi hiyo ya uzalishaji na usafirishaji bidhaa nje ya nchi inakabiliwa na matatizo chungu nzima kutokana na kuharibiwa miundomsingi ya nchi hiyo. Syria imeazimia kushirikiana na baadhi ya mataifa washirika ili kuongeza kiwango cha uzalishaji. Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambayo ilikuwa na mchango usio na mithili katika kuwashinda na kuwasambaratisha magaidi na maadui nchini Syria, imekuwa ikitoa kipaumbele maalumu kwa suala la kuimarisha uhusiano na majirani na mataifa ya eneo hili.

Hapana shaka kuwa, kupanuliwa ushirikiano wa kiuchumi wa Iran na Syria ni bima ya maslahi ya pande mbili na nchi za eneo kwa ujumla. Hati za ushirikiano zilizotiwa saini na pande mbili katika safari ya Rais wa Iran nchini Syria zinaweza sambamba na kiumarisha zaidi ushirikiano wa kimkakati wa nchi mbili zikaondoa pia vizingiti vya sasa na hivyo kufunguliwa ukurasa mpya katika ushirikiano wa nchi mbili.