Rouhani: Matunda makubwa ya JCPOA ni kubatilisha propaganda chafu dhidi ya Iran
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa kushindwa kwa mpango wa kueneza hofu kuhusu Iran kote ulimwenguni ndiyo matunda makubwa zaidi ya makubaliano ya nyuklia kati ya Iran na kundi la 5+1 maarufuku kwa kifupi kama JCPOA.
Rais Rouhani ambaye jana jioni alikuwa akihutubia hadhara ya mabalozi wa nchi za kigeni na wawakilishi wa jumuiya za kimataifa waliko hapa mjini Tehran kwa mnasaba wa maadhimisho ya mwaka wa 37 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu hapa nchini amesema kuwa, baada ya makubaliano hayo ya nyuklia walimwengu walitambua kwamba, propaganda chafu dhidi ya Iran hazina ukweli na kwamba watu wa Iran ni wapenda amani na usalama.
Rais Rouhani amekabidhibisha madai kuwa Iran inataka kulidhibiti eneo la Mashariki ya Kati na kusema: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haikodolei jicho nchi yoyote wana haiingilii mambo ya ndani ya nchi nyingine. Amesema kuwa mapambano halisi dhidi ya ugaidi na kurejesha amani na utulivu katika eneo la Mashariki ya Kati vina umuhimu mkubwa kwa Iran na kwamba Tehran imeazimia vilivyo kupambana na ugaidi na kukomesha machafuko katika eneo hilo. Amewambia mabalozi na wawakilishi wa nchi za kigeni kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iko tayari kushirikiana na nchi zote duniani katika nyanja mbalimbali.
Rais Hassan Rouhani amesema miaka 37 iliyopita wananchi wa Iran walifanya mapinduzi makubwa kwa ajili ya kutaka kujitawala na kuwa huru na kupata ushindi licha ya upinzani wa madola ya kibeberu duniani na kwamba tangu baada ya ushindi huo Iran ilitaka kuwa na uhusiano mzuri na nchi zote duniani.