Jul 06, 2023 07:33 UTC
  • Antonio Guterres
    Antonio Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema katika ripoti yake ya 15 kuhusu azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la umoja huo kwamba: Mapatano ya JCPOA bado ni chaguo bora.

Kulingana na azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la UN kila baada ya miezi sita katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres huwasilisha mara moja ripoti yake katika kikao cha Baraza la Usalama; ambapo ripoti yake ya 14 kuhusu utekelezaji wa azimio hilo na mapatano ya JCPOA iliwasilishwa  Disemba 19 mwaka jana. 

Mapatano ya JCPOA yaliyopasishwa na Baraza la Usalama la UN 

Kikao cha Baraza la Usalama cha kuchunguza ripoti ya 15 ya Antonio Guterres kuhusu azimio nambari 2231 kimepangwa kufanyika leo; ambapo Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa pia atahutubia kikao hicho.  

Antonio Guterres Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika ripoti yake ya 15 kuhusu azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama kuhusu Iran ambalo linatazamiwa kuchunguzwa muda mfupi ujao ameeleza kuwa: Mapatano ya JCPOA bado ni chaguo bora na kuitaka Marekani kuondoa vikwazo dhidi ya Iran na kurefusha mihula ya misamaha katika sekta ya biashara ya mafuta ya nchi hii. 

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ikiwa nchi inayowajibika ilitekeleza ahadi na majukumu yake bila ya dosari au ukiukaji wowote baada ya kusaini mapatano ya JCPOA mwaka 2015 kwa lengo la kuondolewa vikwazo vya kidhalimu vya Washington. Suala hili limethibitishwa pia katika ripoti 16 za Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA). 

Hata hivyo baada ya Donald Trump kuingia White House Januari 2017 na baada ya hatua kadhaa za utangulizi, hatimaye alichukua uamuzi na msimamo wa upande mmoja kinyume na vipengee vya JCPOA, na tarehe 8 Mei mwaka 2018 akaiondoa Marekani kinyume cha sheria katika mapatano hayo na kurejesha vikwazo dhidi ya Iran.  

Tags