Jul 13, 2023 07:52 UTC
  • Katibu Mkuu wa mkutano wa kuiunga mkono Intifadha ya Palestina; Njia pekee ya taifa la Palestina ni kuendeleza muqawama

Katibu Mkuu wa Mkutano wa kuiunga mkono Intifadha ya Palestina amesema kuwa njia pekee liliyonayo taifa la Palestina ni kuendeleza mapambano hadi ushindi wa mwisho.

Sayyid Mojtaba Abtahi amekutana pambizoni mwa mkutano wa mabunge ya Asia hapa Tehran na Ali Faisal Naibu Spika wa Bunge la Palestina na ambaye pia ni mwakilishi wa ofisi ya kisiasa ya harakati ya Kidemokrasia ya Palestina. 

Katika mazungumzo hayo, pande mbili zimechunguza matukio ya karibuni huko Palestina na uvamizi wa karibuni wa Wazayuni huko Jenin. Aidha wamesisitiza kuhusu uungaji mkono mkubwa wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa wananchi na muqawama wa Palestina.  

Sayyid Mojtaba Abtahi na Ali Faisal pia wamesisitiza kuhusu umoja baina ya makundi ya Palestina na kusema: Njia pekee walionayo wananchi wa Palestina ni kuendeleza mapambano hadi kupatikana ushindi. 

Faisal na Sayyid Mojtaba Abtahi pia wametilia mkazo kuendeleza ushirikiano wa kibunge na wabunge kunufaika na uzoefu na uwezo wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge); na kutaka kuendelezwa mawasiliano baina ya mabunge ya Iran na Palestina. 

Ali Faisal sambamba na kuishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa uungaji mkono wake endelevu kwa wananchi wa Palestina amesisitiza kuwa: Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi na serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na wananchi Waislamu na Wanamapinduzi wa Iran wamefungua ukurasa mpya wa mapambano ya wananchi wa Palestina kwa kuiunga mkono Palestina. 

Ali Faisal, Naibu Spika wa Bunge la Palestina 

Tags