-
Rais Pezeshkian: Iran inalenga kuimarisha uhusiano na Oman
Nov 19, 2025 03:29Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesifu uhusiano imara kati ya Iran na Oman, na kueleza kuwa Tehran ina imani kwamba uhusiano wa pande mbili utaendelea kukua kwa "nguvu na uthabiti.
-
Bin Salman: Tunajaribu kupatanisha baina ya Iran na Marekani
Nov 18, 2025 23:19Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudi Arabia ambaye kimsingi ndiye kiongozi nambari moja wa nchi hiyo amesema: "Tutafanya kila tunavyoweza kuhakikisha kunafikiwa makubaliano kati ya Iran na Marekani; (ninaamini kwamba) Tehran pia iko tayari kusaini makubaliano hayo."
-
Iran yapendekeza mfumo wa malipo wa kidijitali katika Jumuiya ya Shanghai
Nov 18, 2025 22:54Mohammad Reza Aref Makamu wa Kwanza wa Rais wa Iran amependekeza kuanzisha mfumo wa pamoja wa malipo ya kidijitali ili kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi 10 wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO).
-
Vipi mauzo ya Iran kwa Afrika yamevunja rekodi katika nusu ya kwanza ya mwaka 1404 Hijria Shamsia?
Nov 18, 2025 08:37Mauzo ya bidhaa za Iran barani Afrika yaliongezeka maradufu katika miezi sita ya kwanza ya mwaka huu (1404 Hijria Shamsia), na kufikia dola milioni 675.
-
Araghchi: Sheria za kimataifa bado “zipo hai” licha ya kushambuliwa
Nov 18, 2025 07:56Waziri wa mambo ya nje wa Iran amesisitiza ujumbe wa mkutano wa kimataifa kuhusu sheria za kimataifa, akisema mkutano huo umeonyesha dhamira ya Tehran ya kutetea haki mbele ya mashambulizi ya kigeni.
-
Iran yatoa mkono wa pole kwa India kufuatia kuaga dunia ajalini mahujaji wa nchi hiyo huko Saudi Arabia
Nov 18, 2025 07:54Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Esmaeil Baqaei ametuma salamu za rambirambi kwa familia za mahujaji wa ibada ya Umrah wa India waliofariki dunia katika ajali ya basi nchini Saudi Arabia.
-
Iran: Lazima IAEA idumishe uadilifu wa kiufundi na kutoegemea upande wowote kisiasa
Nov 17, 2025 23:19Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) lazima utimize maagizo uliyokabidhiwa ya kiufundi, ujiepushe na mielekeo ya kisiasa, na kukataa mashinikizo yanayotolewa na Marekani na washirika wake wa Ulaya.
-
Iran yalaani mauaji na ukiukaji wa haki za binadamu unaondelezwa na Israel huko Gaza na Ukingo wa Magharibi
Nov 17, 2025 05:46Iran imelaani vikali mauaji yanayoendelea kufanywa na utawala wa Israel dhidi ya Wapalestina pamoja na ukiukaji wa wazi wa haki za binadamu katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi.
-
Mahitaji ya dhahabu ya Iran yafikia tani 58 Jan–Sep, yashika nafasi ya tano duniani
Nov 17, 2025 05:42Iran imekuwa ni ya tano duniani kwa mahitaji ya dhahabu katika kipindi cha robo tatu za kwanza za mwaka huu, ikichochewa na ongezeko la uagizaji wa dhahabu ili kueneza akiba ya Benki Kuu ya taifa hili.
-
Araghchi: Iran lazima ijiimarishe ili kujilinda kwenye ‘Msitu’ ulioundwa na Marekani
Nov 16, 2025 23:45Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amekemea Marekani kwa kuchochea mashindano ya silaha duniani kupitia matumizi ya mabavu waziwazi na uvunjaji wa sheria za kimataifa, akisema hakuna njia nyingine ila kujiimarisha katika “msitu” ulioundwa na Washington.