-
Orban: Hungary haitaruhusu Ukraine kujiunga na EU miaka 100 ijayo
Jan 23, 2026 23:17Waziri Mkuu wa Hungary, Viktor Orban amesema kwamba Ukraine inajaribu kushawishi na kuathiri matokeo ya uchaguzi ujao wa bunge nchini Hungary, akisitiza kuwa nchi yake haitaruhusu Ukraine kujiunga na Umoja wa Ulaya katika miaka 100 ijayo.
-
Kwa nini rais wa Brazil amemkejeli Trump?
Jan 23, 2026 23:17Rais Lula da Silva wa Brazil amemkejeli Rais Donald Trump wa Marekani kutokana na tweet nyingi za kutatanisha anazoandika katika mitandao ya kijamii.
-
Imamu wa Swala ya Ijumaa Tehran: IRGC ndiyo nguzo kuu ya kuwalinda wananchi na Mapinduzi ya Kiislamu
Jan 23, 2026 11:19Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran, Hujjatul Islam Walmuslimin Haj Ali Akbari, amezungumzia matukio ya hivi karibuni na mashambulizi ya maadui kwenye maeneo mbalimbali yakiwemo ya ya kidini na kusisitiza kuwa: Maadui walidhani kwamba wangeweza kulilazimisha taifa la Iran kurudi nyuma na kudhibiti mitaa na viwanja kupitia vitisho na kuzusha hofu, lakini wananchi ambao ndio wamiliki halisi wa nchi hii, walijitokeza kwenye medani na kukabiliiana ipasavyo na fitina hiyo.
-
IRGC: Mashirika 10 ya ujasusi yaliilenga Iran baada ya Vita vya Siku 12
Jan 23, 2026 10:43Shirika la Ujasusi la Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetoa taarifa likisema, machafuko ambayo yamekuwa yakifanyika nchini tangu mwishoni mwa Desemba yalikuwa sehemu ya "fitina iliyopangwa" na mashirika ya ujasusi ya nchi 10 maadui, kwa shabaha ya kuivuruga nchi kupitia vitendo vya vurugu, hujuma na kampeni za upotoshaji zilizoratibiwa kwa vyombo vya habari.
-
Umoja wa Mataifa: Walowezi wa Kizayuni wamewaua Wapalestina 240 Ukingo wa Magharibi
Jan 23, 2026 10:16Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imetangaza katika ripoti yake kwamba mwaka jana (2025) walowezi na jeshi la Israel waliua Wapalestina 240 katika Ukingo wa Magharibi.
-
Afrika Kusini kujiondoa katika kundi la G20 wakati wa urais wa Marekani
Jan 23, 2026 09:11Waziri wa fedha wa Afrika Kusini, Enoch Godongwana, amethibitisha kwamba nchi hiyo itaachana na ushirikiano wake na kundi la mataifa tajiri na yale yanayoinukia kiuchumi duniani G20 wakati wa urais wa Marekani katika kundi hilo.
-
Kainerugaba : Ghasia za baada ya uchaguzi nchini Uganda zamesababisha vifo vya watu 30
Jan 23, 2026 08:47Mkuu wa Jeshi la Uganda na mwana wa Rais aliyechaguliwa tena, Yoweri Museveni, amesema leo Ijumaa kwamba wafuasi 30 wa upinzani wameuawa na 2,000 wamekamatwa kufuatia uchaguzi wa karibuni nchini humo.
-
Ubepari; unyonyaji wa maliasili na shinikizo kwa mazingira
Jan 23, 2026 04:41Ubepari, kama mojawapo ya mifumo mikuu ya kiuchumi katika ulimwengu wa sasa, umeundwa kwa kuzingatia ulimbikizaji wa mtaji, faida na upanuzi wa masoko usio na kikomo.
-
Rais Pezeshkian: Mpango wa maadui wa Umma wa Kiislamu ni kueneza ugaidi na machafuko
Jan 23, 2026 04:07Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, mpango wa maadui wa Umma wa Kiislamu ni kueneza na kuendeleza ugaidi na ukosefu wa usalama katika eneo kwa kuzusha migogoro ya ndani katika mataifa ya Kiislamu.
-
Russia: Wananchi wa Iran wamesambaratisha njama za maadui
Jan 23, 2026 04:07Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Russia amesema kuwa, machafuko ya hivi karibuni nchini Iran yalifadhiliwa waziwazi kutoka nje ya nchi.