-
Umoja wa Afrika waiondolea vikwazo Guinea
Jan 23, 2026 04:06Umoja wa Afrika umetangaza kuiondolea vikwazo Guinea ilivyoiwekea kufuatia mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 2021, baada ya nchi hiyo kuandaa uchaguzi wa rais mwezi Disemba.
-
Abdul-Malik Al-Houthi: Baraza la Amani la Trump ni kifuniko tu cha satwa na uporaji
Jan 23, 2026 04:06Sayyed Abdul Malik al-Houthi, kiongozi wa harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema kuwa, baadhi ya nchi zinaweka mashinikizo makubwa ya kiuchumi kwa watu wa Yemen kwa kuchelewesha kwa makusudi kuwasili meli na kubainisha kwamba Baraza la Amani la Trump ni kifuniko tu cha satwa na uporaji.
-
CDC: Mlipuko wa Mpox barani Afrika sio dharura tena ya kiafya
Jan 23, 2026 04:05Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa barani Afrika (CDC) ametangaza kuwa, mlipuko wa Mpox barani Afrika kwa sasa sio "dharura ya kiafya barani humo.
-
Qalibaf: Jaribio la mapinduzi na ugaidi wa karibuni ni mwendelezo wa Vita vya Siku 12
Jan 23, 2026 00:19Spika wa Bunge la Iran amesema kwamba vitendo vya kigaidi vya hivi karibuni nchini Iran vilikuwa kiungo cha mwisho cha Vita vya Siku 12, na kwamba utawala wa Kizayuni wa Israel na Marekani ziliwaunga mkono magaidi waliowaua raia wa Iran, polisi na askari usalama.
-
Ripoti: Zaidi ya raia 370 waliuawa Kivu, mwezi Desemba 2025
Jan 23, 2026 00:19Imeelezwa kuwa, zaidi ya raia 370 waliuawa Kivu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwezi Disemba mwaka jana.
-
Save the Children: Sudan inapitia kipindi kirefu zaidi cha kufungwa shule duniani
Jan 22, 2026 23:52Shirika la Save the Children limeonya kwamba vita vinavyoendelea nchini Sudan vimewanyima elimu watoto zaidi ya milioni 8, katika kile kinachoelezwa kama kipindi kirefu zaidi cha kufungwa shule duniani.
-
Tovuti ya Israel: Ujerumani inaendelea kufadhili mauaji ya kimbari huko Gaza
Jan 22, 2026 23:52Tovuti ya Israel, 972+ imechapisha ripoti ndefu ya uchunguzi kuhusu uhusiano wa kijeshi kati ya Ujerumani na Israel, ikihitimisha kwamba mauzo ya silaha ya Ujerumani yameendelea kumiminika Israel licha ya madai kwamba yamesitishwa kutokana na mauaji ya kimbari ya watu wa Gaza.
-
'Bodi ya Amani' ya Trump ni aina ya ukoloni mamboleo
Jan 22, 2026 23:51Mkuu wa Jamaat-e-Islami Pakistan (JIP) ametangaza kwamba "Bodi ya Amani" iliyotangazwa na Rais wa Marekani, Donald Trump kusimamia utawala wa eneo la Palestina la Ukanda wa Gaza ni aina mpya ya mfumo wa ukoloni mamboleo. Bodi hiyo ni taasisi inayojumuisha watu kama Tony Blair, mmoja wa wahusika wakuu wa mauaji ya mamilioni ya watu wa Iraq.
-
Iran, mshirika mkuu wa kibiashara wa Afghanistan; uagizaji wa Kabul kutoka Tehran wapanda hadi dola bilioni 3.45
Jan 22, 2026 23:50Kiwango cha mabadilishano ya biashara kati ya Iran na Afghanistan kinaongezeka. Serikali ya Taliban imetangaza kuwa, uhusiano wa kibiashara kati ya Iran na Afghanistan umeongezeka hadi dola bilioni tatu na nusu.
-
Muqawama wa Yemen na ufafanuzi mpya wa mlingano wa nguvu katika Bahari Nyekundu
Jan 22, 2026 08:11Vyombo vya habari vya utawala ghasibu wa Israel sanjari na kuchapisha ripoti mbalimbali, vimekiri juu ya taathira ya operesheni za vikosi vya muqawama vya Yemen kwa uchumi wa utawala huo.