-
Risasi za Israel zapatikana katika miili ya watoto waliouawa wakati wa ghasia hivi karibuni Iran
Jan 22, 2026 07:03Risasi za kiwango cha kijeshi zinazohusishwa na jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel zimepatikana katika uchunguzi wa kitabibu wa miili ya watoto waliouawa na magaidi wakati wa ghasia za hivi karibuni zilizochochewa na serikali za kigeni nchini Iran
-
Jeshi la Iran la IRGC laionya Marekani na Israel dhidi ya makosa yoyote ya kimahesabu
Jan 22, 2026 07:03Kamanda Mkuu wa Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amewaonya maadui dhidi ya kufanya makosa yoyote ya kimahesabu, akisisitiza kwamba vikosi vyake viko tayari kutekeleza maagizo ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyyed Ali Khamenei.
-
Lavrov: Ufaransa na Ukraine zinasaidia makundi ya kigaidi barani Afrika
Jan 22, 2026 07:01Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia, Sergey Lavrov, amesema kuwa Ufaransa na Ukraine zinatoa msaada kwa makundi ya kigaidi na mitandao ya waasi barani Afrika, ikiwemo matawi ya magaidi ISIS au Daesh.
-
Mauritius yamwambia Trump: ‘Hakuna Mjadala’ kuhusu Chagos
Jan 22, 2026 07:01Umiliki wa Mauritius juu ya Visiwa vya Chagos hauna utata wowote na “haupaswi tena kuwa mada ya mjadala,” amesema Mwanasheria Mkuu wa taifa hilo la pwani ya Afrika Mashariki. Gavin Glover alitoa kauli hiyo akijibu matamshi ya Rais wa Marekani, Donald Trump, kuhusu uamuzi wa Uingereza kukabidhi tena udhibiti wa eneo hilo la Bahari ya Hindi kwa koloni lake la zamani.
-
Guinea‑Bissau yapanga uchaguzi wa urais na bunge Desemba 6
Jan 22, 2026 07:00Serikali ya mpito za Guinea‑Bissau zilitangaza Jumatano kwamba uchaguzi wa urais na ule wa wabunge utafanyika tarehe 6 Desemba mwaka huu, hatua inayoweka ratiba rasmi ya kwanza ya uchaguzi tangu mapinduzi ya kijeshi ya Novemba 2025. Tangazo hilo linachunguzwa kwa karibu na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS), ambayo imekuwa ikisisitiza kipindi kifupi na jumuishi cha mpito.
-
Kamanda mwandamizi wa Jeshi la Iran amuonya vikali Trump
Jan 22, 2026 03:26Kamanda wa ngazi ya juu wa jeshi la Iran amemuonya vikali Rais Donald Trump wa Marekani kufuatia matamshi yake ya hivi karibuni ya vitisho dhidi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei.
-
Iran yatangaza idadi ya waliouawa katika ghasia zilizochochewa na maajinabi
Jan 22, 2026 02:32Wakfu wa Mashahidi na Maveterani wa Iran umetangaza katika taarifa kwamba, "katika vitendo vya hivi karibuni vya ugaidi vilivyoungwa mkono na Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel, watu 3117 walipoteza maisha yao, wakiwemo raia na maafisa usalama."
-
Wanajeshi 8 wa Nigeria wauawa katika shambulio la Boko Haram Borno
Jan 22, 2026 02:32Wanajeshi wanane wa Nigeria wameuawa huku wengine 50 wakijeruhiwa baada ya wapiganaji wa genge la kigaidi la Boko Haram kushambulia kambi ya kijeshi katika jimbo la Borno, kaskazini mashariki mwa nchi.
-
Putin: Denmark imekuwa ikiitazama Greenland kama koloni lake
Jan 22, 2026 02:31Rais wa Russia, Vladimir Putin amesema, Denmark imekuwa ikiichukulia Greenland kama koloni lake. Amesema hayo akitoa mtazamo wake kuhusu mpango wa Rais wa Marekani, Donald Trump wa 'kukinunua' kisiwa hicho cha Aktiki kinachojitawala.
-
Bunge la EU lasimamisha makubaliano ya biashara na US; kisa vitisho vya Trump
Jan 22, 2026 02:21Bunge la Ulaya limesimamisha rasmi mchakato wa kuidhinisha makubaliano yake ya kibiashara na Marekani, kutokana na vitisho vya Rais Donald Trump vya kutoza ushuru wa asilimia 10 kwa bidhaa za EU zinazoenda Marekani, iwapo umoja huo hautaafiki azma ya Washington ya kuitwaa Greenland.