-
Wizara ya Usalama ya Iran yawatia mbaroni magaidi 2 wa MKO walioshiriki katika ghasia za Tehran
Jan 19, 2026 08:07Wizara ya Usalama ya Iran imetangaza kuwa imewatia nguvuni mamluki wawili wenye mfungamano na kundi la kigaidi la Munafiqin (MKO). Mamluki hao walikuwa wapiongozwa na kupewa maagizo la uongozi wa kundi hilo wenye makao yake nchini Ujerumani.
-
Qalibaf: Vita vya karibuni vya kigaidi dhidi ya Iran vinafanana na shambulio la pager la Israel huko Lebanon
Jan 19, 2026 08:05Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) Muhammad Baqer Qalibaf amesema kuwa "Vita vya kigaidi vya mtindo wa Daesh" vya hivi karibuni hapa nchini vilikuwa na malengo sawa na ya shambulio la kigaidi la Israel dhidi ya Lebanon mwezi Septemba mwaka 2024.
-
Afrika Kusini yatangaza janga la kitaifa kufuatia mvua na mafuriko yaliyouwa watu 30
Jan 19, 2026 08:05Afrika Kusini imetangaza janga la kitaifa kutokana na mvua kubwa na mafuriko ambayo yamesababisha vifo vya takriban watu 30 kaskazini mwa nchi hiyo, kuharibu maelfu ya nyumba na kusomba barabara na madaraja.
-
Nigeria yauwa magaidi 40 wa Boko Haram katika operesheni za anga
Jan 19, 2026 08:04Jeshi la Anga la Nigeria limetangaza kuwua limeuwa takriban magaidi 40 wa Boko Haram katika mashambulizi ya anga mtawalia iliyofanya mapema wiki hii katika jimbo la Borno kaskazini mashariki mwa Nigeria.
-
Rached Ghannouchi Kiongozi wa Ennahda Tunisia atimiza siku 1,000 jela
Jan 19, 2026 08:00Rached Ghannouchi kiongozi wa chama cha Kiislamu chenye ushawishi mkubwa nchini Tunisia cha al-Nahdha na Spika wa zamani wa bunge la nchi hiyo jana Jumapili alitimiza siku 1,000 akiwa kifungoni jela. Ghannouchi ametaja kifungo kinachomkabili kuwa ni " wakati wa mahesabu ya kisiasa."
-
Ulimwengu wa Spoti, Jan 19
Jan 19, 2026 05:17Hujambo msikilizaji mpenzi, na karibu tutupie jicho baadhi ya matukio makubwa ya spoti yaliyojiri ndani ya siku zilizopita, ikiwemo fainali ya michuano ya AFCON. Nakusihi tuwe sote hadi tamati ya kipindi…..Karibu…….
-
Kuimarishwa uhusiano wa Iran na Iraq; njia ya pamoja ya kufikia utulivu endelevu katika eneo
Jan 19, 2026 03:56Viongozi wa ngazi za juu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kikao na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iraq wamesisitiza umuhimu wa kustawishwa na kuimarishwa ushirikiano wa pamoja baina ya nchi mbili kwa shabaha ya kudhamini uthabiti wa eneo.
-
Makanisa ya al-Quds yaonya kuwa ‘Uzayuni wa Kikristo’ unahatarisha Ukristo
Jan 19, 2026 03:50Viongozi wakuu wa Kikristo katika mji wa Palestina wa al-Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na Israel, wameonya kuwa “Uzayuni wa Kikristo” pamoja na ajenda za nje zinavunja umoja wa Wakristo katika Ardhi Takatifu na kudhoofisha mamlaka yao ya kiroho na kijamii.
-
Afisa wa UN: Sudan 'imetumbukia katika shimo la mateso makubwa yasiyoelezeka'
Jan 19, 2026 03:50Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, ametahadharisha kuhusu kuzorota kwa hali ya haki za binadamu na kibinadamu nchini Sudan, kufuatia ziara yake ya siku tano katika nchi hiyo inayokumbwa na vita.
-
Iran yawakamata vinara 300 wa ghasia zilizochochewa kutoka nje ya nchi
Jan 19, 2026 03:49Wizara ya Usalama ya Iran imesema kuwa zaidi ya watu 300 ambao ni vinara wakuu na waratibu wa ghasia za hivi karibun nchini, ghasia ambazo zimechochewa na madola ya kigeni, wamekamatwa.