-
Baraza la Usalama wa Taifa: Wafanya uharibifu watachukuliwa hatua bila ya kuonewa huruma
Jan 10, 2026 00:56Baraza la Usalama wa Taifa la Iran limetoa taarifa, -ambayo mbali na kuashiria kuwa tangu baada ya vita vya siku 12 Marekani na utawala wa kizayuni wa Israel hazijaacha kufanya chokochoko za vita na uadui dhidi ya taifa la Iran-, imesisitiza kwamba: taifa linaloheshimika la Iran litazivunja mbinu za kihujuma na ufanyaji uharibifu wa adui kwa umoja na mshikamano wa kitaifa.
-
Araqchi: Teknolojia haiwezi kuangamizwa kupitia mashambulizi
Jan 10, 2026 00:55Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameashiria mashambulizi ya utawala wa Kizayuni na Marekani dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran vinavyofanya kazi kwa malengo ya kiraia katika vita vya siku 12 na kusema baadhi ya majengo, taasisi na suhula za nyuklia zinazotumika kwa malengo ya amani za Iran zilidhurika hata hivyo teknolojia haiweza kuangamizwa kupitia mashambulizi.
-
HAMAS: Tuko tayari kukabidhi uendeshaji wa Ghaza kwa kamati ya shakhsia wa kujitegemea
Jan 09, 2026 23:04Msemaji wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema, harakati hiyo ilishaamua tokea huko nyuma kwamba haitakuwa na ushiriki wa moja kwa moja katika hatua yoyote ya upangaji wa masuala ya kiidara na kiuendeshaji ya siku za usoni katika Ukanda wa Ghaza.
-
Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati amwalika Rais Putin baada ya ushindi
Jan 09, 2026 23:03Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Faustin-Archange Touadera, ambaye hivi karibuni ametangazwa mshindi katika uchaguzi wa rais, amemwalika Rais Vladimir Putin wa Russia kutembelea nchi hiyo jambo linaloashiria azma yake ya kushirikiana na Russia.
-
Ukosoaji mkali zaidi kuwahi kufanywa na Ujerumani: Marekani inaigeuza dunia "pango la wezi"
Jan 09, 2026 23:02Rais Frank-Walter Steinmeier wa Ujerumani amezikosoa vikali sera za nje za Rais wa Marekani Donald Trump na kuutaka ulimwengu usiruhusu nidhamu ya dunia ikageuzwa kuwa "pango la wezi".
-
Wazimu wa kijeshi wa Marekani; Bajeti ya kijeshi ya dola trilioni 1.5 kwa mwaka 2027
Jan 09, 2026 23:02Rais Donald Trump ametangaza kwamba anakusudia kuongeza bajeti ya kijeshi ya Marekani hadi dola trilioni 1.5 ifikapo mwaka 2027.
-
Marekani ina ndoto gani kuhusu mafuta ya Venezuela?
Jan 09, 2026 10:52Kufuatia operesheni ya kijeshi ya Marekani dhidi ya Venezuela, swali muhimu limeibuka: Washington ina mipango gani kwa ajili ya mafuta ya nchi hiyo?
-
Khatibu wa Sala ya Ijumaa: Waandamanaji watajitenga na wachache wanaovuruga amani
Jan 09, 2026 09:40Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo ya mjini Tehran, Hujjatul Islam Sayyid Mohammad Hassan Abu Torabi Fard amesema, waandamanaji waelewa na wenye ghera ya uhuru na mamlaka imara ya nchi watatenganisha njia yao na ya wachache wanaoitakia mabaya nchi, wafanyao vitendo vya ukatili na kuvuruga nidhamu ya jamii; na hilo ni jambo lenye ulazima usioweza kuepukika.
-
Russia yashambulia viwanda vya kuunda droni za kijeshi nchini Ukraine
Jan 09, 2026 07:33Jeshi la Russia, katika kujibu hujuma ya Ukraine dhidi ya makao ya Rais Vladimir Putin, limetekeleza mashambulizi kadhaa dhidi ya vituo vya kuunda ndege za kivita zisizo na rubani au droni nchini Ukraine.
-
Nchi za Kiislamu zapinga safari za waziri wa Israel katika eneo la Somalia la 'Somaliland'
Jan 09, 2026 07:32Nchi 22 za Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) zimetoa taarifa na kutenga zinapinga vikali kujitenga eneo la Somaliland la Somalia huku zikilaani vikali safari ya waziri wa mambo ya nje wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika eneo hilo.