Khatibu wa Sala ya Ijumaa: Waandamanaji watajitenga na wachache wanaovuruga amani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i135290-khatibu_wa_sala_ya_ijumaa_waandamanaji_watajitenga_na_wachache_wanaovuruga_amani
Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo ya mjini Tehran, Hujjatul Islam Sayyid Mohammad Hassan Abu Torabi Fard amesema, waandamanaji waelewa na wenye ghera ya uhuru na mamlaka imara ya nchi watatenganisha njia yao na ya wachache wanaoitakia mabaya nchi, wafanyao vitendo vya ukatili na kuvuruga nidhamu ya jamii; na hilo ni jambo lenye ulazima usioweza kuepukika.
(last modified 2026-01-31T16:06:48+00:00 )
Jan 09, 2026 13:10 UTC
  • Khatibu wa Sala ya Ijumaa: Waandamanaji watajitenga na wachache wanaovuruga amani

Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo ya mjini Tehran, Hujjatul Islam Sayyid Mohammad Hassan Abu Torabi Fard amesema, waandamanaji waelewa na wenye ghera ya uhuru na mamlaka imara ya nchi watatenganisha njia yao na ya wachache wanaoitakia mabaya nchi, wafanyao vitendo vya ukatili na kuvuruga nidhamu ya jamii; na hilo ni jambo lenye ulazima usioweza kuepukika.

Hujjatul Islam Abu Torabi Fard amesema: "katika siku za hivi karibuni tumekabiliwa na matukio machungu", na akafafanua kwamba, inapasa kuwepo na mazingatio maalumu kwa madukuduku yaliyotolewa, ukosoaji uliofanywa na njia za ufumbuzi zilizopendekezwa na wadau wa kiuchumi hususan wafanyabiashara wa baazar ambao ni miongoni mwa sekta za uchumi zenye taathira kubwa zaidi nchini Iran.

Khatibu wa Sala ya Ijumaa ameendelea kubainisha: "sambamba na kutoa shukurani kwa hima iliyoonyeshwa na viongozi juu ya suala hili muhimu natilia mkazo ulazima na umuhimu wa kuandaa mipango mwafaka ya kuufanya uchumi wa nchi uwe thabiti".

Aidha, amesema, kutenganisha kwa uelewa kati ya wakosoaji na maandamano ya malalamiko ya umma kwa upande mmoja na wavurugaji nidhamu na usalama wa jamii kwa upande mwingine ni jukumu muhimu sana la kijamii kwa ajili ya kulinda usalama, mshikamano na kuchukua hatua za kuondokana na ugumu na mapungufu yaliyopo.

Hujjatul Islam Abu Torabi Fard amesisitiza kwamba, waandamanaji waelewa na wenye ghera ya uhuru na mamlaka imara ya nchi watatenganisha njia yao na ya wachache wanaoitakia mabaya nchi, wafanyao vitendo vya ukatili na kuvuruga nidhamu ya jamii; na hilo ni jambo lenye ulazima usioweza kuepukika. 

Katika sehemu nyingine ya khutba zake, Khatibu na Imamu wa muda wa Sala ya Ijumaa ya leo hapa mjini Tehran ameashiria pia matamshi ya kifidhuli na kipuuzi yaliyotolewa na rais wa Marekani na waziri mkuu wa utawala wa kizayuni kuhusiana na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na akasema, inavyoonekana wawili hao wameghafilika na somo walilofunzwa kutokana na namna taifa adhimu la Iran lilivyojihami kwa nguvu na uwezo kamili katika vita vya siku 12 na kibao kikali walichozabwa kwenye nyuso zao chafu.../