-
Kwa nini Marekani imepoteza nafasi yake ya kimataifa?
Jan 02, 2026 23:08Gazeti la The Wall Street Journal limeandika katika ripoti yake kwamba: "Marekani imepoteza hadhi yake ya kimataifa kwa kiasi kikubwa katika miaka 25 ya kwanza ya karne ya 21, kutokana na utawala mbaya, vita vya gharama kubwa na migogoro ya ndani."
-
Al-Jazeera: Israel inajiandaa kuanzisha tena mashambulizi makali Gaza
Jan 02, 2026 23:07Waziri wa Vita wa Israel, Israel Katz ameliagiza jeshi la utawala huo haramu kujiandaa kurejea kwenye mapigano makali dhidi ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas katika Ukanda wa Gaza, hayo yameripotiwa na kanali ya televisheni ya al-Jazeera ikinukuu gazeti la Kizayuni la The Jerusalem Post.
-
Sheikh Mayunga, mwanazuoni mashuhuri wa Kiislamu Afrika Mashariki ameaga dunia
Jan 02, 2026 09:58Jamii ya Kiislamu Afrika Mashariki na hasa nchini Tanzania imekumbwa na msiba mkubwa kufuatia kufariki dunia kwa mwanazuoni mashuhuri, na mfasiri wa Qur'ani Tukufu, Sheikh Ali Jumaa Mayunga, aliyefariki dunia tarehe 1 Januari 2026, jijini Dar es Salaam, Tanzania.
-
Khatibu wa Sala ya Ijumaa: Adui anatamani kuyageuza matatizo ya kiuchumi kuwa mgogoro wa kiusalama
Jan 02, 2026 09:25Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran amesema maadui wa Iran wanajaribu kutumia matatizo ya kiuchumi ili kuibua mzozo wa kiusalama nchini
-
Onyo kuhusu matokeo mabaya ya vitisho vya Marekani dhidi ya mpango wa nyuklia wa amani wa Iran
Jan 02, 2026 08:59Tehran imeonya kuhusu matokeo mabaya ya vitisho vya hivi karibuni vya Marekani dhidi ya mpango wa nyuklia wa amani wa Iran.
-
Wairani wamkumbuka na kumuenzi Haj Qassem Soleimani
Jan 02, 2026 07:29Maelfu ya watu kutoka Iran na kote ulimwenguni wamekusanyika katika mji wa Kerman ulioko kusini mwa Iran, kuadhimisha kumbukizi ya kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem, aliyekuwa kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC.
-
Iran yajibu bwabwaja, vitisho na matamshi ya uingiliaji ya Trump
Jan 02, 2026 06:47Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran ameonya kwamba, uingiliaji kati wa Marekani katika masuala ya ndani ya Jamhuri ya Kiislamu utavuruga utulivu wa eneo zima la Asia Magharibi na kuhatarisha moja kwa moja maslahi ya Marekani katika eneo.
-
Wahamiaji kadhaa wakufa maji katika ajali ya boti Gambia
Jan 02, 2026 06:44Askari wa gadi ya baharini ya Gambia wameopoa majini miili saba ya wahamiaji wasio na vibali, huku wengine 96 wakiokolewa kufuatia ajali ya boti pwani ya nchi hiyo.
-
Ethiopia yawarejesha nyumbani zaidi ya raia 27,000 waliokwama nje ya nchi
Jan 02, 2026 06:43Serikali ya Ethiopia imetangaza kwamba imewarejesha nyumbani zaidi ya raia 27,300 waliokuwa wamekwama katika nchi za Myanmar na Saudi Arabia katika kipindi cha miezi mitano iliyopita.
-
Denmark: Tutasimama kidete dhidi ya mpango wa Trump kwa Greenland
Jan 02, 2026 06:43Waziri Mkuu wa Denmark, Mette Frederiksen amepinga vikali juhudi mpya za Marekani za kuinunua Greenland, akitoa hotuba kali dhidi ya mpango huo, huku mvutano wa kidiplomasia baina ya pande mbili hizo ukipamba moto.