-
Denmark: Tutasimama kidete dhidi ya mpango wa Trump kwa Greenland
Jan 02, 2026 06:43Waziri Mkuu wa Denmark, Mette Frederiksen amepinga vikali juhudi mpya za Marekani za kuinunua Greenland, akitoa hotuba kali dhidi ya mpango huo, huku mvutano wa kidiplomasia baina ya pande mbili hizo ukipamba moto.
-
Jackie Chan amwaga machozi kuwalilia watoto wa Ghaza
Jan 02, 2026 03:27Jackie Chan, muigizaji maarufu wa Hollywood na filamu za Hong Kong, amewaga machozi kuwalilia watoto wa Ghaza akielezea huzuni yake kubwa kutokana na hali mbaya ya kibinadamu katika ukanda huo akitangaza kwamba alipotazama video ya mahojiano na mtoto wa Palestina alilia na kumkumbusha tena mateso yasiyoisha ya watoto wa Ghaza.
-
Jenerali Vahidi: Vitisho vya Maadui vinatokana na woga na hofu yao
Jan 02, 2026 03:24Naibu kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH, amesisitizia wajibu wa kuendelea Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuunga mkono Mhimili wa Muqawama na kusema kuwa: "Vitisho na bwabwaja za maadui zinatolewa kutokana na woga na hofu waliyo nayo na hazitaathiri njia ya Jamhuri ya Kiislamu na ya Kambi ya Muqawama."
-
Fat’h: Hatua zozote za kikanda bila ya kutatua kadhia ya Palestina zitashindwa tu
Jan 02, 2026 03:24Mmoja wa viongozi waandamizi wa harakati ya ukombozi wa Palestina ya Fat’h amesema kuwa, Makubaliano ya Abraham ni udanganyifu wa kisiasa na hayatoleta utulivu katika eneo hili maadamu yanapuuza kadhia ya Palestina.
-
Karibu dola bilioni 50, deni la taifa la Libya
Jan 02, 2026 03:23Deni la taifa la Libya lilikuwa ni karibu dola bilioni 50 za Marekani mwaka 2024, hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya kila mwaka ya Ofisi ya Ukaguzi ya Libya, ambayo huwa inatolewa mwishoni mwa kila mwaka unaofuata.
-
Tatizo Kubwa la Mwaka Mpya duniani ni Trump
Jan 02, 2026 03:23Gazeti moja la nchini Uingereza limeufungua mwaka mpya wa 2026 kwa ripoti kuhusu wasiwasi juu ya hali ya mashindano ya Kombe la Dunia ya mpira wa miguu mwaka huu 2026 na kusema kuwa rais wa Marekani Donald Trump ni tatizo kubwa kwa mashindano hayo.
-
Pezeshkian: Jenerali Soleimani alikuwa nembo ya maelewano na utiifu kwa Kiongozi Muadhamu
Jan 01, 2026 23:18Rais Masoud Pezeshkian amesisitiza kwamba, taifa la Iran litaendeleza njia ya Shahid Luteni Jenerali Qassem Soleimani aliyekuwa kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH na viongozi wengine wa kambi ya Muqawama akiongeza kuwa, shahidi Soleimani alikuwa nembo ya maelewano, huruma na utiifu kwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.
-
Baraza la Makanisa Duniani lataka kuwekewa vikwazo Israel kutokana na vita vya Gaza
Jan 01, 2026 23:18Baraza la Makanisa Duniani (WCC) limeutaka Umoja wa Ulaya (EU) kuiwekea Israel vikwazo vikiwemo vya silaha kutokana na mauaji ya kimbari yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni huko Gaza, na ukiukaji wa haki dhidi ya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan unaokaliwa kwa mabavu.
-
Jeshi la Somalia laangamiza makumi ya magaidi wa al-Shabaab
Jan 01, 2026 23:17Makumi ya wanamgambo wa kundi la kigaidi la al-Shabaab lenye misimamo ya kufurutu ada , wameangamizwa katika operesheni ya wanajeshi wa Somalia.
-
DRC: Watu 1,500 wameuawa mashariki mwa nchi
Jan 01, 2026 23:17Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imesema zaidi ya raia 1,500 wameuawa katika ghasia zinazoendelea katika jimbo la Kivu Kusini, mashariki mwa nchi hiyo tangu mapema mwezi Desemba, 2025 mpaka sasa.