-
Rais Pezeshkian akutana na Kiongozi Muadhamu anapoanza mwaka wake wa tatu madarakani
Aug 10, 2026 03:20Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Masoud Pezeshkian, amekutana na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei, ikiwa ni mwanzo wa mwaka wake wa tatu tangu aingie madarakani.
-
Iran yazindua teknolojia ya virusi vya kuangamiza saratani
Aug 10, 2026 03:17Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imezindua teknolojia ya kiasili kwa ajili ya kubuni, uhandisi wa kijeni, uzalishaji wa virusi vya oncolytic vinavyoua seli za saratani.
-
Jeshi la Yemen laangamiza makumi ya mamluki wa Saudia mkoani Ta'izz
Aug 10, 2026 03:15Msemaji wa Vikosi vya Jeshi la Yemen amesema vitengo vya kijeshi vya nchi hiyo vimeendesha operesheni kubwa dhidi ya vibaraka wa Saudia katika mkoa wa kusini-magharibi wa Ta’izz, na kuwaua na kuwajeruhi makumi yao.
-
DRC yajipanga kwa sensa ya kwanza ya kitaifa baada ya miaka 42
Aug 10, 2026 03:12Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) inajiandaa kufanya sensa yake ya kwanza ya kitaifa baada ya zaidi ya miongo minne, kazi kubwa inayolenga kuwapatia hadhi rasmi mamilioni ya raia ambao wameishi bila vitambulisho vya kitaifa vilivyotolewa na serikali.
-
Wanajeshi wasiopungua 10 wauawa katika shambulio katikati mwa Mali
Aug 10, 2026 03:09Wanajeshi wasiopungua 10 waliuawa jana Jumapili katika shambulio lililofanywa katika kambi ya jeshi katikati mwa Mali. Kundi moja la kigaidi lenye mfungamano na mtandano wa al Qaida limedai kuhusika na hujuma hiyo.
-
Araqchi: Mazungumzo na Oman kuhusu Lango-Bahari la Hormuz yako katika hatua za mwisho
Aug 09, 2026 11:09Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema leo kwamba mazungumzo na Oman kuhusu Lango Bahari la Hormuz yako katika hatua za mwisho na kuongeza: "Bila shaka, hii haina maana kwamba Lango la Hormuz litafunguliwa. Ufunguzi wa Lango la Hormuz unategemea masharti mengine."
-
Mamia ya watu wanaandamana Afrika Kusini kupinga chuki dhidi ya wageni
Aug 09, 2026 11:04Mamia ya watu wameandmana katika miji mbalimbali nchini Afrika Kusini wakitaka kukomeshwa ghasia dhidi ya wahamiaji, ambazo zimewalazimisha makumi ya maelfu ya watu kukimbia nchi hiyo.
-
Mwanzilishi mwenza aonya: Wikipedia imekuwa chombo cha propaganda cha CIA, taasisi zingine zenye nguvu
Aug 09, 2026 11:02Mwanzilishi mwenza wa Wikipedia, Lawrence Mark Sanger, ameonya kwamba ensaiklopidia hiyo ya mtandaoni imekuwa chombo cha propaganda, akisema Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) na marekebisho yanayofanywa na makampuni mbalimbali kwenye Wikipedia yamedhoofisha sera yake ya kutopendelea upande wowote.
-
Yemen yavishambulia vituo vya nishati vya Saudi baada ya nchi hiyo kukiuka anga ya Sa’adah na Hajjah
Aug 09, 2026 11:00Yemen imeishambulia miundombinu ya nishati ya Saudi Arabia ikiwa ni jibu kwa ndege zisizo na rubani za adui zinazokiuka anga ya mikoa ya Sa’adah na Hajjah huko Yemen.
-
Wabunge Kenya: Hakuna makubaliano mapya ya ushirikiano wa kijeshi na Uingereza
Aug 09, 2026 10:20Wabunge wa Kenya wamesema kuwa hakuna makubaliano mapya yaliyofikiwa kati ya Kenya na Uingereza kuhusu mkataba wa ushirikiano wa kijeshi (BATUK).