-
Zolqadr: Lango-Bahari la Hormuz litaendelea kufungwa hadi pale Marekani itakapobadilisha tabia yake
Aug 09, 2026 09:55Afisa wa ngazi ya juu wa usalama wa Iran kwa mara nyingine tena amesisitiza kuwa nchi hiyo haitalegeza vikwazo vya usafirishaji kupitia Lango Bahari la Hormuz hadi pale Marekani itakapobadilisha mwenendo wake mbele ya Tehran.
-
Kwa nini Trump amekwama katika "fedheha ya kimkakati" katika vita dhidi ya Iran?
Aug 09, 2026 05:43Gazeti la Financial Times, huku likinukuu wachambuzi mashuhuri, linaripoti kuwa Trump amekwama katika "fedheha ya kimkakati" kuhusiana na vita dhidi ya Iran na kwamba hawezi kujiondoa katika hali hiyo bila kulipa gharama za kisiasa nchini kwake.
-
Mshauri wa Kiongozi Mkuu Iran asema vikosi vya Marekani lazima viondoke Asia Magharibi, ahimiza ushirikiano wa kikanda
Aug 09, 2026 03:17Mshauri mkuu wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ali Akbar Velayati, amesema vikosi vya majeshi ya kigeni lazima viondoke Asia Magharibi, akitaja uwepo wao wa kama chanzo kikuu cha ukosefu wa usalama na utulivu katika eneo hilo.
-
Malaysia na Indonesia zasisitiza kuunga mkono Palestina na maeneo matakatifu Baytul-Muqaddas
Aug 09, 2026 03:15Malaysia na Indonesia kwa mara nyingine tena zimesisitiza uungaji mkono wao kwa watu wa Palestina na kuhifadhi hadhi ya maeneo matakatifu ya Kiislamu na Kikristo katika Baytul-Muqaddas inayokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel.
-
Afrika Kusini yaadhimisha Maandamano ya Wanawake ya 1956 – mapambano ya uhuru bado yanaendelea
Aug 09, 2026 03:00Afrika Kusini, leo Jumapili, inaadhimisha miaka 70 tangu Maandamano ya Wanawake ya 1956, wakati wanawake wapatao 20,000 wa mbari na rangi zote walipoandamana hadi mji mkuu wa utawala, Pretoria, kupinga sheria za ubaguzi wa rangi zilizowalazimisha wanawake weusi kubeba vibali vilivyowazuia kutembea.
-
UNICEF yachukua hatua dhidi ya afisa anayetuhumiwa kufanya ujasusi kwa maslahi ya Israel
Aug 09, 2026 02:58Msemaji wa Umoja wa Mataifa amethibitisha kwamba Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) linachukua hatua dhidi ya mmoja wa wafanyakazi wake, kufuatia madai kwamba alifanya ujasusi kwa maslahi ya Israel wakati wa kazi yake ya awali katika Shirika la Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa.
-
Jenerali wa Trump anatafuta njia ya kujiondoa vitani na Iran huku machaguo ya kijeshi ya Marekani yakipungua
Aug 09, 2026 02:54Mkuu wa Majeshi ya Marekani, Jenerali Daniel Caine, amewasihi maafisa wakuu wa utawala wa Trump kutafuta njia ya kupunguza vita na Iran, akionya kwamba ongezeko zaidi la mapigano ya kijeshi haliwezi kupata mafanikio makubwa na kwamba linawaweka wanajeshi wa Marekani na washirika wake katika hatari ya majibu angamizi ya Iran.
-
Pezeshkian akumbuka mashambulizi ya mabomu ya atomiki huko Hiroshima na Nagasaki, asema mtazamo uleule bado unatawala Washington
Aug 08, 2026 12:59Rais Masoud Pezeshkian wa Iran amelaani mashambulizi ya mabomu ya nyuklia yaliyofanywa na Marekani dhidi ya miji ya Hiroshima na Nagasaki huko Japan na kueleza kuwa mtazamo fikra zilizopelekea kufanyika mashambulizi hayo bado zipo Washington hii leo.
-
Maafisa wa ngazi ya juu wa Iran wapongeza nafasi ya waandishi wa habari katika kuhami ukweli na umoja wa kitaifa
Aug 08, 2026 12:57Maafisa wa Iran wamewasifu na kuwapongeza waandishi wa habari kutokana na mchango wao wa kukabiliana na taarifa potofu za uhasama na vita vya kisaikolojia, na kusisitiza umuhimu wa vyombo vya habari katika kulinda uelewa wa umma na umoja wa kitaifa.
-
UN: Watoto zaidi ya 300 wamefariki dunia kwa Ebola tangu kuanza mlipuko huo huko Kongo
Aug 08, 2026 12:55Watoto zaidi ya 300 wamefariki dunia kutokana na ugonjwa wa Ebola tangu mlipuko huo uliopoikumba Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Idadi hii ni kwa mujibu wa takwimu zilizotangazwa jana Naibu Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Farhan Haq.