-
Ansarullah: Baraza la Usalama la UN limepoteza hadhi; maazimio yake hayana thamani
Aug 08, 2026 12:50Kiongozi mwandamizi wa harakati ya Ansarullah nchini Yemen amepuzilia mbali hatua ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ya kulaani mashambulizi ya makombora ya kulipiza kisasi dhidi ya Saudi Arabia na meli za kibiashara za utawala huo wa kifalme akisema kuwa chombo hicho cha kimataifa kimepoteza uhalali na hadhi yake, na maazimio yake hayana thamani yoyote.
-
Russia yashambulia eneo la kutengeneza makombora na ghala la mafuta la Ukraine huko Kyiv
Aug 08, 2026 12:46Wizara ya Ulinzi ya Russia imetangaza kuwa vikosi vya ulinzi ya nchi hiyo vimeshambulia kituo cha kijeshi na viwanda cha Ukraine kinachotengeneza makombora ya cruise pamoja na ghala la mafuta huko Kyiv.
-
Tabia za Marekani Kudumisha Mvutano katika uhusiano wake na Iran
Aug 08, 2026 06:28Mwenendo wa Rais Donald Trump wa Marekani kuhusiana na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran unachochea kuendelea kwa mvutano na uhasama katika uhusiano wa Washington na Tehran.
-
Iran yayaasa mataifa ya Kiislamu: Ni wakati sasa wa sisi kujitegemea, kuwa na udugu wa kweli
Aug 08, 2026 03:24Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa wito wa kuwepo muunganiko na ushirikiano mkubwa wa kikanda, ikitilia mkazo udharura wa mataifa ya eneo kutegemea uwezo wao wa kikanda ili kuondoa uingiliaji wa kigeni.
-
Telegraph: Vita dhidi ya Iran vinaweza vikawa moja ya makosa ya kihistoria
Aug 08, 2026 03:22Gazeti la Telegraph linalochapishwa nchini Uingereza limekiri katika ripoti yake kwamba Marekani na Israel zimeshindwa katika vita, huku Iran ikiwa imeibuka mshindi, na kwamba vita hivi vinaweza kuwa tukio muhimu sana la kupelekea kupungua satua na ushawishi wa Marekani duniani.
-
Uturuki, Saudi Arabia na Pakistan zasaini mkataba wa pamoja wa ulinzi huku nguvu ya Marekani ikipungua
Aug 08, 2026 02:46Saudi Arabia imesaini makubaliano ya pamoja ya ulinzi kati yake na Uturuki Pakistan kwa lengo la kuimarisha usalama wa pamoja na ushirikiano wa kijeshi huku nguvu za kijeshi za Marekani zikipungua katika eneo hili.
-
Wakulima wa Kenya wakanusha madai ya matumizi ya sianidi baada ya tembo 15 kufa huko Amboseli
Aug 08, 2026 02:43Wakulima wanaopakana na Hifadhi ya Taifa ya Amboseli nchini Kenya wamekanusha kutumia sianidi baada ya tembo 15 kufariki dunia baada ya kudaiwa kuwa tembo hao wamekufa kutokana na sumu hiyo.
-
Mlipuko wa Ebola Kongo wapindukia maambukizi 4,000
Aug 08, 2026 02:42Idadi ya kesi za Ebola zilizothibitishwa hadi kufikia jana Ijumaa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zilikuwa zimepindukia 4,000 huku maeneo ya afya yaliyoathirika yakiongezeka.
-
Mashambulizi mapya ya Yemen yaangamiza mamluki wa Saudia wasiopungua 58
Aug 07, 2026 13:39Vikosi vya ulinzi vya Yemen vimefanya operesheni kubwa iliyozilenga ngome za kijeshi na vituo vikuu vya kamanda za kijeshi zilizokuwa zikisimamiwa na mamluki wanaoungwa mkono na Saudi Arabia nchini humo.
-
Mkuu wa Mossad awatimua maafisa wawili wakuu kwa kufeli mpango wa kuipindua serikali ya Iran
Aug 07, 2026 12:29Mkuu wa shirika la ujasusi na ugaidi la utawala wa kizayuni wa Israel Mossad, Roman Gofman, amewafukuza kazi maafisa wawili wakuu wa intelijensia baada ya kushindwa au kutotekelezwa mpango wa kuipindua serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.