-
Hungary: Mpango wa EU wa kuiba mali za Russia ni 'tangazo la vita'
Dec 16, 2025 03:00Waziri Mkuu wa Hungary, Viktor Orban ametahadharisha kuwa, hatua yoyote ya Umoja wa Ulaya ya kutwaa milki na fedha za Russia zilizozuiliwa bila idhini ya Budapest ni kukiuka sheria za Ulaya na itakuwa sawa na "tangazo la vita."
-
ISIL yatangaza kuhusika na shambulio baya nchini Syria
Dec 16, 2025 02:55Kundi la kigaidi la ISIL (Daesh) limedai kuhusika na shambulio baya lililolenga vikosi vitiifu kwa Abu Mohammad al-Jolani nje kidogo ya Idlib, kaskazini magharibi mwa Syria.
-
M23 yaendelea kuwashikilia mamia ya askari wa Burundi
Dec 16, 2025 00:36Kundi la waasi wa M23 linalodaiwa kuungwa mkono na Rwanda limewakamata mamia ya wanajeshi wa Burundi wakati wa mashambulizi yake ya hivi punde mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, afisa wa kundi hilo amesema, huku mapigano yakiendelea mashariki mwa DRC.
-
Iran: Madai ya kumiliki visiwa vya Ghuba ya Uajemi ni dhidi ya mamlaka ya kujitawala na ujirani mwema
Dec 15, 2025 23:58Iran imesema kuwa madai yoyote ya kumiliki visiwa vitatu vya Ghuba ya Uajemi yaani Tomb Kubwa, TombNdogo na Bu Musa ni ukiukaji wa kanuni za ujirani mwema na kutoheshimu mamla ya kujitawala ya nchi nyingine.
-
ICC yatupilia mbali rufaa ya Israel ya kuomba waranti wa kumkamata Netanyahu ubatilishwe
Dec 15, 2025 23:57Kitengo cha rufani cha Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC kimetupilia mbali hoja za utawala wa kizayuni wa Israel za kupinga uhalali wa uchunguzi wa mahakama hiyo kuhusu jinai zilizofanywa Ukanda wa Ghaza kufuatia vita vya kinyama na vya mauaji ya kimbari ambavyo utawala huo haramu ulivianzisha Oktoba 7, 2023 dhidi ya Wapalestina wa ukanda huo uliowekewa mzingiro.
-
Mvua kubwa na mafuriko yaua watu 37 katika mji wa Safi, Morocco
Dec 15, 2025 23:22Wizara ya Mambo ya Ndani ya Morocco leo JUmatatu imetangaza kuwa mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa yamesababisha vifo vya takriban watu 37 katika mji wa pwani wa Safi nchini humo.
-
Makaburi ya Waislamu nchini Australia yanajisiwa baada ya ufyatuaji risasi huko Sydney
Dec 15, 2025 23:21Makaburi ya Waislamu nchini Australia yamenajisiwa kwa vichwa vya nguruwe vilivyokatwa kufuatia ufyatuaji risasi uliolenga hafla ya Kiyahudi mjini Sydney nchini humo.
-
ECOWAS yapinga mpango wa mpito wa kijeshi wa Guinea-Bissau
Dec 15, 2025 23:21Viongozi wa Afrika Magharibi wamepinga mpango wa mpito uliotangazwa na watawala wa kijeshi wa Guinea-Bissau, badala yake wametaka kurejea haraka kwa utaratibu wa kikatiba. na kuonya kuhusu vikwazo vinavyolengwa dhidi ya wale wanaozuia mchakato huo.
-
Ana kazi lakini ana njaa; kwa nini wazazi wa Uingereza wanatafuta misaada ya chakula?
Dec 15, 2025 23:20Kadiri uchumi wa Uingereza unavyozidi kulegea na kuporomoka, takribani robo ya wazazi wenye ajira nao wanalazimika kutafuta msaada wa chakula cha bure kutoka mashirika ya hisani.
-
Mkutano wa Tehran; Ubunifu wa Iran kwa ajili ya mwafaka wa kikanda na uthabiti wa Afghanistan
Dec 15, 2025 11:29Mkutano wa wawakilishi maalum wa nchi jirani za Afghanistan pamoja na Russia umefanyika katika wizara ya mambo ya nje ya Iran, mjini Tehran.