-
Iran: IAEA haina haki ya kutaka kukagua vituo vilivyoshambuliwa
Dec 15, 2025 08:05Mkuu wa shirika la nyuklia la Iran amekosoa wito wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA wa kufanya ukaguzi mpya kwenye maeneo ya nyuklia yaliyoshambuliwa, akisisitiza kwamba taasisi hiyo ya UN haina itifaki zilizo wazi za kukagua maeneo ambayo yalishambuliwa na utawala wa Israel na Marekani.
-
Majirani za Afghanistan wapinga uingiliaji wa kigeni, vikwazo
Dec 15, 2025 08:04Wawakilishi maalum wa nchi majirani za Afghanistan wamepinga vikali uwepo wowote wa kijeshi wa maajinabi, wakizitaka nchi zilizopelekea kushuhudiwa mgogoro wa sasa nchini humo kuchangia ujenzi mpya bila kutumia msaada kama chombo cha kisiasa.
-
Wahajiri wa Kiafrika waaga dunia kwa baridi mpaka wa Morocco, Algeria
Dec 15, 2025 07:31Wahamiaji tisa wa Kiafrika wamepoteza maisha kutokana na baridi kali karibu na mpaka wa Morocco na Algeria.
-
IRGC: Maadui watakabiliwa na mwelekeo mpya wa uwezo wa Iran iwapo wataanzisha vita
Dec 15, 2025 07:30Msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC Ali-Mohammad Naeini amesema kwamba ikiwa vita vitazuka, adui atakabiliwa na viwango vipya na vya hali ya juu vya nguvu ya kijeshi ya Jamhuri ya Kiislamu.
-
Yemen yaonya kuhusu kushtadi jinai za Israel Gaza, Ukingo wa Magharibi
Dec 15, 2025 07:29Wizara ya Mambo ya Nje ya Yemen imetahadharisha dhidi ya kuongezeka kwa ukatili unaofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina huko Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan unaokaliwa kwa mabavu, ikiukosoa utawala huo pandikizi kwa kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano na kuzidisha mashambulizi.
-
Ulimwengu wa Spoti, Dec 15
Dec 15, 2025 07:25Hujambo mpenzi mskilizaji na karibu tuangazie baadhi ya matukio makubwa yaliyojiri viwanjani ndani ya siku saba zilizopita kote duniani.
-
Shujaa Muislamu aliyejitolea kupambana na gaidi kuwaokoa Mayahudi Australia + VIDEO
Dec 15, 2025 03:26Shujaa Muislamu ambaye video yake imeenea mno mitandaoni ikimuonesha akijitolea kwenda katikati ya ufyatuaji risasi na kujikubalisha kupigwa risasi lakini aweze kupambana na kumnyang'anya silaha gaidi aliyekuwa anawafyatulia risasi Mayahudi huko Sydney, anaendelea kupongezwa kote duniani na kuambiwa kwamba ni shujaa ambaye kujitolea kwake kumeweza kuoko maisha ya watu wengi.
-
Velayati: Iran inaiunga mkono Hizbullah ya Lebanon kwa dhati
Dec 15, 2025 03:26Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika Masuala ya Kimataifa amesema kuwa, Hizbullah ni moja ya nguzo muhimu zaidi za kambi ya Muqawama na ina jukumu la kimsingi katika kukabiliana na Uzayuni. Hivyo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, chini ya maagizo ya Kiongozi Muadhamu, itaendelea kuiunga mkono harakati hiyo ambayo iko mstari wa mbele katika Muqawama.
-
Zaidi ya watu 500,000 wamekimbia makazi yao katika wiki 2 za mapigano DRC
Dec 15, 2025 03:25Zaidi ya watu 500,000, wakiwemo zaidi ya watoto 100,000, wamekimbia makazi yao tangu Desemba 1 kutokana na mapigano makali katika mkoa wa Kivu Kusini wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Hayo yalitangazwa jana Jumapili na Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF).
-
Maandamano ya fujo yanaendelea nchini Tunisia
Dec 15, 2025 03:23Mamia ya watu nchini Tunisia wameendelea kufanya maandamano yaliyoitishwa na vyama vya upinzani na mashirika ya kisheria. Maandamano hayo yanaendelea kwa wiki ya nne mfululizo kwenye mitaa ya mji mkuu Tunis.