-
Msemaji wa serikali ya Iran: Azimio nambari 2231 limekwisha muda wake
Oct 21, 2025 23:08Fatemeh Mohajerani Msemaji wa serikali ya Iran amesema kuwa azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililoidhinisha makubaliano ya nyuklia ya Iran ya mwaka 2015 limekwisha muda wake na kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelitaarifu Baraza la usalama kuhusu kumalizika muda huo.
-
Teknolojia ya Nyuklia Yazaa Masuluhisho Mapya kwa Mustakabali wa Uchumi wa Iran
Oct 21, 2025 23:05Iran imezindua kituo cha kwanza cha mionzi ya kilimo katika eneo la kaskazini-magharibi, kilichopo Ardabil, hatua inayoonesha dhamira ya taifa kutumia teknolojia ya nyuklia kwa madhumuni ya amani ili kuimarisha usalama wa chakula na kukabili changamoto za kilimo kote nchini.
-
Chuo Kikuu cha Arizona; Taasisi ya saba Marekani kukataa matakwa ya sera mpya ya Trump
Oct 21, 2025 23:03Vyuo Vikuu saba vya juu nchini Marekani vimepinga mpango tata wa "kielimu" wa Ikulu ya White House, ambao unashutumiwa kuwa ni mkakati wa kisiasa unaolenga kuwanyamazisha wapinzani na kuwaadhibu wanaoiunga mkono Palestina katika Vyuo Vikuu.
-
Kwa nini Afrika ni fursa kubwa ya kiuchumi kwa Iran?
Oct 21, 2025 23:01Mkuu wa Jumuiya ya Biashara ya Pamoja ya Iran na Afrika amesema: "bara la Afrika ni hazina iliyofichika ya uchumi wa dunia na fursa kubwa kwa Iran."
-
Rais wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy, aanza kifungo cha miaka mitano jela
Oct 21, 2025 11:25Rais wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy, ameanza kutumikia kifungu cha miaka mitano jela katika gereza moja mjini Paris baada ya kupatikana na hatia ya kufanya ufisadi.
-
Ethiopia ambayo ni mwanachama wa BRICS yaanza mchakato wa kubadili deni la dola kuwa Yuan
Oct 21, 2025 08:58Ethiopia imeanza mazungumzo na China kuhusu kubadili sehemu ya deni lake la dola bilioni 5.38 kuwa mikopo inayotumia sarafu ya yuan, ikiwa ni sehemu ya juhudi za serikali kupunguza shinikizo la fedha za kigeni na kuimarisha uhusiano wa kibiashara.
-
Araghchi na Guterres wajadili migogoro ya Gaza, Yemen
Oct 21, 2025 08:12Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres wamefanya mazungumzo ya simu na kuzungumzia matukio ya kikanda ikiwemo hali ya Gaza na Yemen.
-
Hamas: Israel lazima igharamie ujenzi mpya wa Gaza
Oct 21, 2025 08:01Afisa mwandamizi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas, Mousa Abu Marzouk ametoa wito kwa Israel kufadhili kikamilifu ukarabati na ujenzi mpya wa Ukanda wa Gaza, akitaja uharibifu mkubwa na haki za Wapalestina zaidi ya milioni mbili ambao wamepoteza makazi yao, makazi na riziki.
-
Trump: Ukraine haiwezi kushinda vita dhidi ya Russia
Oct 21, 2025 07:56Rais wa Marekani, Donald Trump amesema haitakidi kwamba Ukraine inaweza kuibuka mshinda katika vita vyake na Russia.
-
Uwanja wa Ndege Khartoum washambuliwa na RSF kabla ya kufunguliwa
Oct 21, 2025 07:29Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) vimeripotiwa kushambulia maeneo muhimu katika mji mkuu wa Sudan, ikiwa ni pamoja na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Khartoum, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya nchi hiyo.